Aachiwe Mbowe peke yake?

Fundi Mchundo

Platinum Member
Joined
Nov 9, 2007
Posts
10,448
Reaction score
8,705
Hivi serikali ikifuta kesi ya Mbowe peke yake Chadema watafanya nini? Watamshauri Mwenyekiti kiti wao asikubali kutoka mpaka wakina Adamoo nao waachiwe? Au watasema atoke ili awaongoze kupambania uhuru wa wanachama wenzake ambao bado wako mahabusu?

Amandla...
 
Ungekuwa mwanachama ungeshauri Nini?
 
Hapo itafutwa hiyo kesi na washtakiwa wote wanakuwa huru

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kama Mbowe anahusishwa na kufadhili ugaidi akionekana hana hatia, iweje wale waliohusishwa na huo ugaidi wawe na hatia?

Muhimu waachiwe wote, sio kumtoa Mbowe na kuwaacha kina Adamoo wasiwe na mtetezi.
 
Wewe uwe wa kwanza wengine wafuatie.
Kesi ni moja, iwapo Kwa mmoja ni bambikizi maana yake ni bambikizi Kwa wote.
Hawawezi kusema hawana ushahidi wa kutosha dhidi ya Mbowe lakini wanao dhidi ya wenzake? Nakumbuka yule binti aliyekuwa mahabusu pamoja na Twaha alitolewa ili apewe ubunge lakini Twaha alibaki akisota.
Nadhani kuna haja ya kubadilisha kauli mbiu iwe " Mbowe na wenzake sio magaidi."

Amandla...
 
Ukiona hivyo ni mambo ya michongo tu.
 
Hapo sio kuachiwa Mbowe, kama Mbowe akitoka maanayake kesi inafutwa na wote wanao husishwa na kesi hiyo automatically wanakuwa hawana kesi ya kujibu.
 
Akina Adamoo ni chambo tu mlengwa ni Mbowe,kwa hiyo mlengwa akishatoka hawatakuwa tena na haja ya chambo!
 
Mkuu Fundi Mchundo , kesi ikifutwa kwa Nolle, ni kesi yote inafutwa na washitakiwa wote wanaachiwa huru!. Hii kesi ya Mbowe imethibitisha Tanzania hatuna kabisa good criminal defence attorneys wa level ya Murtaza Lakha!.

Ingekuwa ni Lakha, saa hizi nolle zamani!. Angemaliza hii kesi day one. Kwa vile kuna uthibitisho kuna mtu anaitwa Lijenje alikamatwa nao na hadi sasa hajulikani alipo, kazi ya kwanza ya Murtaza Lakha ingekuwa ni kuanza kwa kujaza tuu kitu kinaitwa Habeas Corpus, kuomba mahakama, iiamuru serikali kumleta Linjenje mahakamani!. Kesi ingeishia hapo!.
Hawa mawakili waliopo, japo wapo wapo tuu kama wapo, ila kiukweli ni kama hakuna kitu kabisa!.
P
 
Ni kichaa tu anaweza mwachia Mbowe akawabaliza; Hao walikuwa Moshi Kwa ajili ya Mbowe!
 
Kama Mbowe anahusishwa na kufadhili ugaidi akionekana hana hatia, iweje wale waliohusishwa na huo ugaidi wawe na hatia?

Muhimu waachiwe wote, sio kumtoa Mbowe na kuwaacha kina Adamoo wasiwe na mtetezi.
Na lile li pisto na misokoto ya bangi je nayo sio makosa?
 
Kama Mbowe anahusishwa na kufadhili ugaidi akionekana hana hatia, iweje wale waliohusishwa na huo ugaidi wawe na hatia?

Muhimu waachiwe wote, sio kumtoa Mbowe na kuwaacha kina Adamoo wasiwe na mtetezi.

..itabidi waachiwe wote.

..lakini kesi hii ni ya ajabu kidogo.

..serikali inadai kina Adamoo walikiri makosa mwezi August 2020.

..lakini Mbowe anayetuhumiwa kuwa ndiye recruiter, financier, na mastermind, wa ugaidi wamekamatwa July 2021.
 
Mbona utakua upumbavu, kwamba Mbowe afutiwe mashitaka,alafu wakina ADAMOO wabaki ndani,ILIHALI KESI yao wote ni moja
 
Mbona utakua upumbavu, kwamba Mbowe afutiwe mashitaka,alafu wakina ADAMOO wabaki ndani,ILIHALI KESI yao wote ni moja
Si mnaweza kushitakiwa pamoja lakini wengine wakaachiwa kwa kukosa ushahidi na wengine wakatiwa hatiani?

Amandla...
 
Wewe Mzee kwani kuna mahakama kama wakati ule sasa ni michongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…