Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Abbas Kinzasa ndilo jina halisi la Sindano Ndogo Inayoshona Makoti, lakini kutokana na kutotaka kujivimbisha kichwa akajiita asilimia ndogo ama asilimia ishirini kwa lugha ya Kimasai, mwite 20%
Binafsi, nilimfahamu kupitia kipindi cha redio ya Maajabu ama iite Magic FM, kijulikanacho kama BAMIZA ambapo goma lake liitwalo MONEY lilipigwa karibia kila siku.
Nikamsikia kwenye kolabo lake na Bushoke huku wakililia suala la ndoa za kuchaguliwa na wazazi kisha nikamsikia kwenye MONEY.
Kwa mara ya kwanza, nilimwona kwenye video ya MAISHA YA BONGO.
Miaka ikaenda na hatimaye, jina lake likazidi kuziteka nyoyo za wapenda muziki mzuri.
20 alisugua sana soli pale kwa Roy ( G Records) lakini akili yote ya Roy ilikuwa kwa Blue ambaye alikuwa wa moto sana (katikati ya 2003 mpaka 2005)
20 alipita Backyard Records na kuangusha NAFICHA chini ya mikono salama ya BRYTON.
20 aliangusha mkwaju mmoja na STEVE MWEUPE "STEVE WHITE" uliitwa WHY, bonge moja la mdude. Abbas kalia sana humo.
Baada ya kufanya kazi zote hizi na kukuza jina kwa kiasi fulani, kitu kikawa kitu pale 20 alipokutana na MAN WALTER.
YA NINI MALUMBANO na TAMAA MBAYA zilikuwa nyimbo za taifa mpaka bwana Abbas akajibebea TUZO TANO za Kili ndani ya USIKU MMOJA na kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kufanya hivyo.
TUZO TANO za Bwana Abbas hazikuibua maneno yoyote kwa kuwa wote waliona ALISTAHILI lakini kuna bwana alibeba TUZO TATU, ikasemekana kuwa zilikuwa za kupangwa, eti huyo bwana alijiandaa na kwenda ukumbini na suti tatu tofauti ambazo kila suti moja ilivaliwa alipopokea TUZO MOJA. Wakati TUZO za 20 zinatangazwa 20 alikuwa na Afande Sele mkoani, kwenye ndinga wakienda kupiga show na TUZO zikapokelewa na Man Walter.
Baada ya tuzo, 20 akawa JUU MNOOOOO na hapo ndipo mambo yalipoharibikia. Waandishi wakamfuata na kumsema kuwa alijiweka kihuni, hakuwa na mwonekano wa KISTAA na mboyoyo MINGI.
Huo ukawa mwanzo wa anguko la Abbas.
Mambo yakawa si mambo baada ya MTAYARISHAJI wake wa karibu,.Man Walter kulipika dude la bwana BONNY MWAITEGE lililoitwa NJOO UFANYIWE MAOMBI kulia kama ilivyolia midundo ya TAMAA MBAYA na YA NINI MALUMBANO. 20 akamaindi sana lakini hakujua kuwa DUNDO ni Mali ya MTAYARISHAJI.
20 akaingia kwenye bifu na Walter na kuandika ngoma ambazo kwa mtazamo wangu naona zililenga kumtoa nishai Walter. Ngoma kama SUBIRA na MBAYA HANA SABABU.
20 akapotea lakini baadaye akaibukia kwa NAS B na kufanya mabalaa kama NG'OMBE WA MASKINI, ikiwa ngoma ya NAS B, hapo alifanya KAJENGE, ambayo ilikuwa ngoma ya MACHENJE na migoma mingine ya kwake.
20 ni msimulizi mzuri sana wa hadithi. Sililiza MALI ZA URITHI, SI MWEMA, MAMA NEEMA, na ile "kwani nani alitaka kunitoa roho, penzi likafika mwisho????"
20 pia ni muumini wa mwendelezo wa hadithi kama ile; MONEY akaliendeleza wazo kwenye NIMERUDI SALAMA na NGOMA nyingine pia zinabebana kimaudhui.
Muvi yake ambayo tunaweza kusema ni muvi ya maisha yake ilitumia asilimia kubwa ya nyimbo zake, iliwaliza wengi na ilifanikiwa kujibebea TUZO pia. Zaidi ya hapo, binti aliyetokea humo, ni mwigizaji mkubwa kwa sasa na anamwita 20 "baba"
20 ni NYOTA ILIYOCHOMOZA MCHANA WA JUA KALI la game lililohitaji mwonekano (star look), kiki, uongo, uvujishaji wa picha za utupu, KUVAA nguo za kike na maseke ya namna hii.
Nawaza kama Roy angemfungulia mlango mtoto wa Kimanzichana kwa kipindi kile ambacho game ilitawaliwa na UANDISHI na ngoma zenye ujumbe, hadithi ya 20 ingekuwaje?
Kila nikimsikiliza 20 najihisi nimerudi miaka ya 60, 70, 80 mpaka 90 huko kutokana na UANDISHI, uimbaji na uongeaji wa 20. Jamaa ameitanguliza jamii mbele kwenye KAZI ZAKE lakini jamii ya sasa imeshikiwa akili na wasiotaka mambo hayo.
NYOTA hung'aa gizani ndiyo maana 20 anaonekana si LOLOTE.
Ukiambiwa utaje mashabiki wa 20%, jina langu liwe la kwanza.
LUAH
THE NAME YOU DON'T HEAR MUCH ABOUT
210524