Naomba msaada wenu wanajamii, nina mgonjwa wa ugonjwa wa kisukari hali yake ni mbaya sana. Madakitari wanameamua kumkata miguu.
Tumepata habari za kuwepo hospitali ya Abbas Medical Centre, Kariakoo mtaa wa Swahili/Ndovu ambayo inafanya miujiza ya kuponyesha matatizo ya ugonjwa wa kisukari kwa wagonjwa waliotakiwa kukatwa miguu, lakini baada ya kupata tiba kwenye kituo hiki sasa wanatembea.
Naomba sana, sana kwa yeyote mwenye taarifa za kituo hiki atupatie taarifa kabila hatujaanza safari ya kuja Dar.