The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Abas Mtemvu amewataka wanachama wa CCM wasioteuliwa katika kura za maoni kutulia na kuongeza nguvu kazi kwenye uchaguzi.
Mwenyekiti Mtemvu ameyasema hayo katika ziara ya Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makala wilayani Kigamboni.
Amesema wana-CCM wote waungane ili Chama Cha Mapinduzi kishinde katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ni msingi wa mwaka 2025.
Mwenyekiti Mtemvu amesisitiza wanachama wote ambao majina yao hayajateuliwa wawe na subira na wasihame chama chao kwani CCM ni taasisi kubwa.
SOMA PIA: Matukio ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Ameeleza kuwa ushindi wa Chama Cha Mapinduzi unatokana na uimara, umoja na mshikamano kwa viongozi na wanachama.
Akizungumzia juu ya Mwaka 2025 Mtemvu ameendelea kuunga mkono msimamo wa Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi ya Urais ni Dokta Samia Suluhu Hassan kwa salamu maarufu ya Samia mitano tena.
Ziara ya Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amos Makala inaendelea tena novemba 8 katika wilaya ya temeke kabla ya kuelekea Mkoa wa Pwani kwa siku mbili na kuhitimisha kwa mkutano maalum Mkoani Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar, Abbas Zeberi Mtemvu (Picha hii si ya tukio linaloelezwa katika taarifa hii)