Abbas Tarimba, tafadhali chukua fomu ya urais wa TFF

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,519
Uongozi wa Rais wa sasa Karia umekuwa na mapungufu mengi sana katika soka la Tanzania hivyo ninakuomba Mhe. A. Tarimba uchukue fomu ya Urais ili uokoe jahazi hili la TFF linaloenda kuzama.
 
Tarimba umefunga Uzi kujipigia debe hatukutaki na mbona huridhiki kila kitu unataka wewe bana!

Utawapata wasiifikiria tu. Ulikuwepo Yanga mbona hukufanya la maana mpaka leo wanaganga njaa tu!

Tunaenda na Karia, kaleta mafanikio lukuki kwenye mpira wetu ngazi ya club na timu za taifa
 
Akichukua tutatoa SIRI zake zote Chafu.
 
  • Thanks
Reactions: mmh

Na wewe Karia acha watu wawe huru kugombea bhana! Kwani hiyo TFF ni mali ya babu yako wa kule Mogadishu?
 
Akichukua tutatoa SIRI zake zote Chafu.
Naona kaishachukua..

IMG-20210610-WA0074.jpg
 
IMG_0938.jpg

WATU WA KUBETI HAWARUHUSIWI KUONGOZA MPIRA

Hii ni kwa mujibu wa kanuni za maadili za Shirikisho la soka duniani FIFA, ibara ya 26.

Kiongozi wa mpira akichunguzwa na kubainika kujihusisha na kubeti moja kwa moja au siyo moja kwa moja, atapigwa faini ya faranga za Uswisi 100,000 na kufungiwa miaka mitatu kujihusisha na soka.

Wachezaji, waamuzi, viongozi, mawakala wa wachezaji
na mawakala wa mechi.
 
View attachment 1814622

Kajisumbua tu
 
Kajisumbua tu
Ni ngumu kumtoa Karia ,ameshaweka mizizi ,waliochukua fomu wote wanalalamika kukosa udhamini mikoani kwa sababu kila sehemu wanayofika wanaambia tumeshamdhamini Karia na mdhamini mmoja hawezi kudhamini mara mbili ,Sasa imagine Karia kachukua fomu majuzi Jana lakini waliochukua kabla wamekosa wadhamini
 
Na hii haipo Tanzania tu hata ukienda FIFA au caf kote ni hivyo hivyo
 
Sijaelewa huu uchaguzi. Ni nafasi mbili tu zinazogombewa?
 
Namna hawa akina Karia wanavyokomalia hizi nafasi ni wazi wanapigania maslahi binafsi ya kupiga pesa.

Inatakiwa iwekwe sheria kwamba kila nafasi yoyote ya uongozi lazima mtu asihudumie kwa mihula inayozidi miwili ili kuwadhibiti watu sampuli ya hawa akina Karia.
 
Back
Top Bottom