MT255
JF-Expert Member
- May 3, 2012
- 3,606
- 4,914
ABDALLAH GAMA MPIGA RYTHM MWENYE HISTORIA NDEFU
SINA-shaka wale mashabiki wa DDC Mlimani Park Orchestra Sikinde Ngoma ya Ukae ambao ni vijana wa zamani, watakuwa wanakumbuka mbali kila pale linapotajwa jina la mwanamuziki Abdallah Gama.
Gama ni mkungutaji mahiri wa gitaa la kati, Rhythm, aliyepata kusumbua akili za wapigaji magitaa wengine wengi enzi zile, hususan alipokuwa katika bendi hiyo ya Sikinde.
Nguli huyo ni mmoja miongoni mwa wanamuziki 12 ambao mwaka 1978 walijiengua kwenye kundi la Dar International kwa madai ya kupinga uongozi mbovu wa mmiliki wao, Zachariah Ndabameiye na kuanzisha Sikinde.
Baadhi ya wanamuziki wengine waliochomoka Dar International na kwenda kuanzisha Sikinde wakati huo, walikuwa ni Cosmas Chidumule, Abel Bartazal, Joseph Mulenga, Michael Enock, George Kessy, Machaku Salum, Haruna Lwali na Ibrahim Mwinchande.
Akiwa Sikinde, Gama aliweza kujipatia umaarufu mkubwa, hasa kwa umahiri aliokuwa nao katika kulicharaza ipasavyo gitaa la Rhythm kwenye vibao vingi vya bendi hiyo.
Kadhalika, ni mwanamuziki aliyegusa nyoyo za mashabiki wengi kutokana na tungo zake kadhaa zenye ujumbe mzito, kama vile; Hadija, Dar es Salaam Airport, Maudhi ya Nyumbani, Linda na Nawashukuru Wazazi.
Kwa upande wa Dar International aliyoitumikia kuanzia mwaka 1977, Gama alishiriki kupiga Rhythm kwenye vibao vingi, baadhi yake vikiwa ni Sikitiko, Mwana Rudi Uoe na Mwalimu Nyerere.
Tulimtafuta Gama na kuzungumza nae kwa faida ya wasamomaji, ambapo mwenyewe anaanika mambo mengi kuhusiana na historia yake kimuziki na maisha kwa ujumla.
Baba yangu aliyekuwa fundi cherahani, ndiye aliyenivuta kwenye muziki kwani alikuwa akipiga gitaa lisilitumia umeme, Galaton kujifurahisha na wakati mwingine akiburudisha rafiki zake, anasema Gama.
Gama anasema kuwa, akiwa na umri wa miaka 28, alikuwa tayari anafahamu barabara kukunguta gitaa nabendi yake ya kwanza ilikuwa ni Safari Trippers aliyojiunga nayo mwaka 1973.
Akiwa na Safari Trippers, Gama anasema kuwa, alishiriki kupiga Solo kwenye vibao kadhaa, vikiwamo Ooh Lila na Mateso ambavyo vyote ni makucha ya marehemu Marijani Rajab.
Gama asiyependezwa na tabia ya wanamuziki kuhamahama makundi, anasema, mwaka 1975 alijiunga na bendi ya Tanzania Stars ambayo maskani yake ilikuwa ni katika hoteli ya Margot, iliyokuwa mtaa wa Independence (siku hizi mtaa wa Samora) jijini Dar es Salaam.
Ifahamike pia kuwa, mwaka 1984 Gama aliwahi kuitumikia Bima Lee kwa mwaka mmoja akitokea Sikinde, ambapo hata hivyo alitoka na kurejea tena Sikinde mwishoni mwa mwaka 1985.
Nikiwa Bima Lee nilitunga kibao Fungua Macho, pamoja na kushiriki kucharaza gitaa kwenye vibao kama vile; Makulata na Tujemaso, anasema Gama.
Mwishoni mwa mwaka 1985 aliingia nchini Kenya kwa kupitia bandari ya Tanga na kujiunga na bendi ya Super Mazembe iliyokuwa ikitumbuiza kwenye ukumbi wa Garden Square, jijini Nairobi.
Wengi wanaamini kibao Gama Unisamehe cha Sikinde amekitunga yeye, kama nawe u mmoja kati ya watu hao, basi umekosea, kwani Gama mwenyewe anaeleza hivi:
Kibao kile kimetungwa na Tshimanga Kalala Asossa, tukiwa Zanzibar kwenye shoo, mimi nilikuwa Kiongozi wa Jukwaa, sasa kabla hatujaanza kutumbuiza nilipanda jukwaani na kuwaita wanamuziki kwa kutumia mlio wa gitaa langu.
Gama anaendelea kueleza kuwa, ghafla alimuona Asossa aliyekuwa anapenda kutembea na redio ndogo ya kurekodi sauti, na kurekodi kipande alichokuwa anakipiga kisha akaondoka.
Waliporudi Dar es Salaam, kwenye mazoezi Asossa alikuja na mashairi ya wimbo na kile kipande alichokipiga Gama kule Zanzibar kuanzia muziki wa wimbo huo alioamua kuupa kumbukumbu kwa kuuita Gama Unisamehe.
Mafanikio niliyokwishayapata kwenye muziki ni kutembea nchi nyingi duniani, jambo ambalo sikutarajia hapo kabla, anasema Gama huku akikumbuka ziara yake na bendi ya Malembe Stars nchi za nje.
Gama anayejivunia kusomesha watoto wake wote hadi chuo kikuu, anazikumbuka nchi hizo kuwa ni kama vile; Japan Malaysia, Ufilipino, Pakistan na Misri.
Kwa sasa Gama ambaye ni baba wa watoto wanne; Mgeni, Pili, Hadija na Maimuna, yuko katika bendi ya Excel ya jijini Dar es Salaam, huku akiwa na malengo ya kuanzisha bendi yake binafsi.
Mpango mwingine alionao Gama, ni kurudia kuvirekodi upya vibao vyake vya zamani, alivyovitunga akiwa na bendi za Sikinde na Bima Lee, kutokana na shinikizo la mashabiki wake.
Mwisho.