Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
ABDALLAH TAMBAZA NA MOHAMED SAID PAMOJA NUSU KARNE NA KUMBUKUMBU YA SHAMA
Alhamdulilah.
Picha ya kwanza kushoto ni Abdallah Tambaza na huyo mwingine ni mimi.
Hapo ni Jamhuri Park Nairobi katika All Africa Trade Fair mwaka wa 1972.
Nilikuwa na miaka 20 na Abdallah 22.
Hiyo picha ya pili kushoto ni Abdallah Tambaza tena na huyo mwingine ni Mohamed Said.
Picha hii katupiga mdogo wetu Ghose Makaburi ya Kisutu majuma machache yaliyopita tulipokwenda kwenye maziko ya mwenzetu Bi. Shama tuliokua sote Kariakoo toka udogo wetu na tukawa pamoja siku zote hadi alipotangulia mbele ya haki majuma machache yaliyopita.
Nataka nisema kitu kifupi.
Wakati mimi na Abdallah tunaagana pale makaburini akanieleza wema ambao Shama alimfanyia.
Mimi nimekaa kimya namsikiliza lakini naomba dua kimoyomoyo Allah amlipe ndugu yetu i. Shama kwa mema yake na amtie katika pepo ya Firdaus.
Ilikuwa kila Ijumaa baadhi yetu tukitoka msikitini hasa ikiwa tumesali Msikiti wa Maamur ambao ni jirani na nyumbani kwake tunapita nyumbani kwa Shama tunakwenda pale kula pilau.
Huu ndiyo ulikuwa uradi wa Bi. Shama.
Hii ni kila Ijumaa.
Na kwa hakika ilikuwa nafasi nzuri sana kwetu sisi tuliokuwa sote Dar es es Salaam hii kukutana na kuzungumza.
Bi. Shama masikini ukimkuta pale Mansfield kwenye duka lake la ice cream jua kali ukasema hebu niingie kivulini hapa nimsalimu Shama na nile ice cream nipoze joto...
Ukisha poza roho hataki ulipe inakuwa zogo wewe unashikilia lazima ulipe na yeye hataki kupokea hela zako.
Wateja wengine wanashangaa, kulikoni?
Sasa fikiria umekwenda na kaumu yako yote siku ya sikukuu kuwanunulia watoto ice cream.
Watoto wakiona ice cream mzuka unapanda macho yote yako ukutani zilipowekwa picha za kutamanisha za ice cream.
Umma unapiga order za fujo watoto wamefurahi.
Wamekula ice cream kefu yao sasa unakwenda kulipa.
Shama anakataa kupokea fedha.
Kisa ati siku nyingi hamjaonana na kuwa ice cream wamekula wanae.
Mama Abdul (anajijua) katika hali kama hii baada ya kuvutana kwa muda mrefu akamwambia, ''Shama unanifukuza dukani kwako.''
Shama wala hamsikilizi yeye anatabasamu tu na cash register haifungui.
Hawa watoto hivi sasa na mababa na mama na naamini bado wanakwenda Mansfield na watoto wao (leo ni wajukuu zetu) kula ice cream kwenye duka la Shama.
Hawa wanetu baadhi yao ni baba na mama zao wametangulia mbele ya haki na najizuia kutaja majina kuchelea kuwaliza ndugu zangu.
Lakini kwa kuwa wao ni sehemu ya historia hii wanajua nimewakusudia nani na nani.
Tunamuomba mola wetu mtukufu awarehemu hawa ndugu zetu wote waliotangulia awaghufurie madhambi yao na sisi tunaosubiri atupe mwisho mwema.
Sasa huyu mdogo wetu Ghose aliyetupiga picha hii ni mmoja wa wadogo zetu aliyekulia mitaa ya Kariakoo yeye na ndugu zake na ni watu mashuhuri.
Najiuliza sijui nini kilimpata akatupiga picha hii na usiku siku ile ile akanirushia.
Mashaallah ana mkono mzuri wa kupiga picha.