Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
ABDU FATAH MUSSA MTANGAZAJI WA RADIO TEHRAN IRAN
Ulikuwa mwaka wa 2000 Uchaguzi Mkuu wa Pili baada ya uchaguzi wa kwanza 1995.
Niko Tanga.
Sikumbuki vipi tulifahamiana lakini ninachokumbuka ni kuwa siku moja wakati wa kampeni za uchaguzi zikiendelea alinipigia simu akaitambulisha Sauti ya Iran na yeye mwenyewe kuniomba anihoji kuhusu siasa za Tanzania.
Huu ukawa ndiyo mwanzo wa usuhuba wetu.
Ikawa mara kwa mara ananipigia simu tunafanya mahojiano na mazungumzo yetu yanarushwa na Radio Tehran Iran.
Mimi sikujua.
Nilikuja kujua baadae sana kuwa namna yangu ya kueleza matokeo ya siasa na historia ya Tanzania ilikuwa tofauti sana na namna wengine walivyokuwa wanaeleza.
Radio Tehran Idhaa ya Kiswahili inasikilizwa Arabuni ambako kuna wasemaji Kiswahili wengi.
Sasa baada ya mimi kuwa mmoja wa wachambuzi wa siasa kutoka Tanzania vipindi hivi nilivyokuwa nikifanya na Abdul Fatah vikavutia wasikilizaji wengi.
Radio Tehran Idhaa ya Kiswahili ikapanda chati ikawa iko juu.
Radio nyingine mashuhuri wasikilizaji watasikiliza lakini mwisho watafungua Radio Tehran kusikiliza na wao wana lipi kuhusu taarifa hiyo.
Abdul Fatah ni mtangazaji hodari Mashaallah anayejua kuhoji yale ambayo wewe muhojiwa hukutegemea.
Atakuchukua ngazi baada ya ngazi mnapanda na kila kidato kinazua kisa kipya.
Abdu Fatah anakuwa mwanamasumbwi anaemperemba mpinzani wake amtwange sumbwi litakalomwangusha chini na kumaliza pambano.
Wako wanaoghadhibishwa na maswali chokonozi kipindi kikawaka moto muhojiwa akamaliza hasira zake kwa mtangazaji wakaagana.
Hicho ndicho mtangazaji alichokuwa akikitafuta na kakipata bure kabisa.
Akizima digital yake na kuvua headphones anaangua kicheko cha furaha.
Kapata kipindi burudani kwa wasikilizaji wake.
Milton Obote alimfokea mtangazaji wa BBC na akawakomesha wasimpigie simu tena kumletea upuuzi wao.
Siku hizo mwisho wa uhai wake yuko Zimbabwe.
Abdu Fatah akiniwekea staha lakini akiniangushia makombora mazito.
Miaka ya mwanzo ya vyama vingi toka kurejeshwa siasa za vyama vingi zilikuwa moto hasa Zanzibar.
Uchaguzi wa 1995 CCM Zanzibar ilikuwa imeshindwa uchaguzi na waandishi wengi wakihofu kulieleza hili.
Abdu Fatah ataniperemba kwa upole kabisa kunilainisha tuangalie hali ya baadae ya visiwani.
"Sikiliza Abdu mimi panya sifunzwi kula sufi..."
Atacheka.
Nazungumza na Mswahili tena Mzanzibari.
Keshanifahamu.
Ikawa Radio Tehran inapendeza.
Nilipata mshtuko nilipokutana na Abdu Fatah Tehran akaniambia kuwa yeye shahada yake ni ya Uhandisi.
Huyu ndiye Injinia Abdu Fatah Mussa wa Idhaa ya Kiswahili Radio Iran Tehran.
Abdu Fatah Mussa