Ni nani walimuua Abdul Massoud yule mtangazaji wa RTD kipindi cha michezo miaka ya 80? Nasikia wauaji wake walimfuata nyumbani kwake wakampiga risasi bila kuchukua kitu chochote, aliuliwa kwa kisa gani kama mdau anafahamu the motive behind his execution anijuze.
Haya wakongwe tunakuja.
Abdul Masoudi alikuwa mtangazaji wa redio Tanzania na katibu mwenezi wa Yanga. Wakati huo mfadhili mkuu wa Yanga alikuwa mhindi fulani aliyekuwa akimiliki kampuni ya sabuni ya Bobby Soap wakati huo.
Leo hii sikumbuki tena jina la mhindi mwenyewe, ila ili kuiiimarisha Yanga au kujiimarisha mwenyewe ndani ya Yanga, alimfanya Abdul Masoud kuwa pia meneja masoko wa kiwanda hicho cha Bobby Soap ingawa sina kumbukumbu sahihi ya cheo chake leo.
Sasa katika utendaji wake wa umeneja wa Bobby soap, tuliambiwa kuwa kulikuwa na dili ya mali gafi mafuta ya nazi ambayo yaliuzwa Bobby Soap na wajasilimali nje ya channels za kawaida za Bobby Soap na malipo yake yangechukuliwa na Abdul halafu akawagawie wale wajasiliamali wake.
Unfortunately, ilionekana kuwa baada ya mafuta ya nazi kuwa delivered pale Bobby soap, pesa hazikuwarudia wajasiliamalai walioleta mafuta yale ingawa accounting iliyonyesha kuwa mali ghafi zote zilikuwa zimelipiwa.
Hiyo ndiyo ikasababisha fate ya Abdul Masoud. Gunmen walimuua yeye tu, wala hawakumgusa ndugu yeyote ndani ya familia yake na wala hawakuchukua kitu chochote kutoka nyumbani kwake pale Temeke.
Sijui kama hii imekusaidia