Abdul Nondo awataka Watanzania wote kuungana kukemea utekaji

Abdul Nondo awataka Watanzania wote kuungana kukemea utekaji

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Mwenyekiti wa ngome ya vijana akizungumza na waandishi wa habari leo January 9,2025 amesema kuwa

“Naomba niwaambie watanzania suala la ulinzi na usalama ni jambo ambalo tunapaswa tuungane kwa pamoja kupaza sauti zetu kupinga kukemea haya matendo. Na wala tusiseme kwamba haya matukio yanatokea kwa wakosoaji, viongozi wa vyama, wanaharakati kwamba wewe ambaye si mwanaharakati kwamba upo salama.”

“Kwamba wewe uko ndani ya chama cha mapinduzi unajiona uko salama tunajidanganya sana namna matukio haya yalipofikia sasa hivi sio ya vyama tena yameshavuka mpaka. Tarimo(mfanyabiashara Deogratius Tarimo) hajihusishi kabisa na siasa katekwa, umeona Dunstan hajihusishi kabisa na masuala ya kisiasa katekwa kwa hiyo tunapoendelea kukaa kimya tunazidi kuyalea haya matukio yaendelee kutokea.”

1736421156841.png
 
Back
Top Bottom