mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo taifa, Abdul Nondo, amehoji nia na utayari wa Serikali katika kusaidia vijana wasio na ajira kwa kuwekeza zaidi kwenye mafunzo ya ufundi stadi kupitia vyuo vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
Nondo amesema kuwa licha ya Serikali kugharamia ada kwa 100% katika Programu ya Kukuza Ujuzi kwa Vijana, bado idadi ya wanaonufaika ni ndogo mno ukilinganisha na mahitaji halisi ya vijana wanaotafuta ujuzi.
"Programu hii ni muhimu sana kwa vijana wetu, lakini haionekani kupewa uzito wa kutosha na Serikali. Idadi ya nafasi zinazotolewa ni ndogo sana. Mwaka huu, nafasi zilizotolewa ni 8,000 tu nchi nzima, wakati mahitaji ni makubwa zaidi," amesema Nondo.
Kwa mujibu wa Nondo, mfano hai wa changamoto hiyo ni Don Bosco Vocational Training Centre - Oysterbay jijini Dar es Salaam, ambacho kilitengewa nafasi 250 pekee kwa mwaka huu, lakini kilipokea maombi zaidi ya 8,789 kutoka kwa vijana waliotaka kujiunga na programu hiyo.
"Hii inamaanisha kuwa hata wale 8,000 waliopangwa kupokelewa nchi nzima ni idadi ndogo sana, kwani walioomba nafasi Don Bosco pekee wamezidi idadi hiyo. Hapa kuna tatizo kubwa, ama Serikali haina fedha, ama haioni umuhimu wa programu hii, au sio kipaumbele chake?" amehoji Nondo.
Amesisitiza kuwa badala ya Serikali kubana matumizi, inapaswa kuongeza uwekezaji kwenye vyuo vya ufundi ili kutoa nafasi zaidi kwa vijana, kwani mafunzo haya ni mwarobaini wa tatizo la ajira kwa vijana nchini.
"Kwanini Serikali haiwekezi vya kutosha kwenye vyuo vyake vya ufundi? Kwanini isihakikishe kila wilaya inakuwa na chuo cha ufundi kinachotoa programu hizi kwa vijana?" ameendelea kuhoji.
Kwa mujibu wa Nondo, ikiwa Serikali itaongeza uwekezaji kwenye vyuo vya ufundi, vijana wengi zaidi wataweza kupata ujuzi na hatimaye kujiajiri au kupata ajira rasmi, badala ya kuendelea kubaki mitaani bila fursa.
Jambo