Baada ya kufanya vyema pale Coastal Union Abdul Sopu na Victor Akpan walikua "keki moto" kwenye dirisha la usajili wote wakiwaniwa na timu tatu kubwa Tanzania ila Simba ikafanikiwa kumpata Akpan huku Sopu akienda Azam Fc kwa dau linalokadiriwa kua M100.
Baada ya kusajili usajili uliokua unaongelewa sana ni Victor Akpan kwenda Simba huku wachambuzi wengi kama Ally Kamwe, Privaldinho na Shaffih Dauda kuusifia sana ila mambo yamekua ndivyo sivyo Akpan ameshindwa kuonyesha makali ameishia benchi na sasa yupo Jukwaani.
Abdul Sopu nae alianza kwa kukaa benchi Azam Fc huku akionekana kama ataishia kutolewa kwa mkopo kutokana na kukosa namba ila kwa magoli yake mawili dhidi ya Timu bora zaidi kwenye Ligi Kuu inadhirisha kijana huyu ataendelea kua "undisputed starter" kwenye kikosi cha Azam Fc namuona akijitoa kwenye kivuli cha Victor Akpan ambaye duru zinasema atatolewa kwa mkopo mwishoni mwa msimu huu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.