Abdul Sykes anamkabidhi Julius Nyerere chama cha TANU 1954

Abdul Sykes anamkabidhi Julius Nyerere chama cha TANU 1954

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
ABDULWAHID KLEIST SYKES ANAMKABIDHI JULIUS KAMBARAGE NYERERE CHAMA CHA TANU 1954

''Chama cha TANU kama vuguvugu la siasa kilikuwa katika fikra za Abdulwahid kwa miaka mingi na alijitahidi sana kufanya bidii kuona kuwa TANU inaundwa.

Chama ambacho kitawaunganisha wananchi wote bila ya kujali kabila au dini sasa kilikuwa hakizuiliki tena."

Mohamed Said (1998)

''Nilikuwa na swali kuhusu nani khasa walikuwapo katika mkutano na kushiriki wa kuibadili TAA kuwa TANU.

Baba (Abdul Sykes) akashauri kuwa tuombe miadi na Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere ili anipe ukweli niliokuwa nautafuta na kusadikisha mambo mengine yanayohusiana na historia hiyo.

Hivyo tukaenda Msasani kuonana na Mwalimu Jumamosi moja asubuhi.

Kama ilivyotegemewa Mwalimu alifurahi sana kutuona maana ilikuwa muda mrefu watu hawa waliokuwa marafiki wakubwa sana kupata kuonana.

Mwalimu alitoa ushirikiano mkubwa sana kwangu kupata ukweli kutoka kwake katika yale niliyotaka kujua kutoka kwake.

Hii ndiyo ilikuwa siku yao ya mwisho kuonana.''

Aisha ''Daisy'' Sykes (2018)

 
Detective...
Hakuna kitu ni kwa kuwa naijua historia hii na hawa ni wazee wangu na nikaona si watu wengi wanajua tulikotoka nimeona nina wajibu na dhima ya kuihifadhi historia ya harakati za uhuru kwa faida ya wale ambao hawaijui.

Ikiwa umeghadhibika kwa kusoma haya haikuwa nia yangu kukuudhi kwani haikunipitikia kuwa kuna mtu atachukizwa na historia nzuri ya uzalendo kama hii.
 
Mzee

Inaonekana umefikia ukomo wa kujifunza historia ya Dunia ndiyo maana yapo matukio mengi tu umeshindwa kuyajuza wasomaji wako

Kwa mfano masuala ya Magaidi kule Msumbiji, Unyanyasaji wasichana wa kazi kule Arabuni, Vurugu za Masuni na Mashiha kule Middle East, Masuala ya haki za Wakinamama kule afghaAfghan n.k

It's seems kitu Kikubwa ulichokariri ni masuala ya Sykes pekee
 
Kichwa Cha habari kama yalivyo maelezo hayajitoshelezi na yaonekana ni mawazo au mitazamo ya watu

Ungetupa maelezo rasmi yanayoendana na Kichwa cha habari japo kina mapungufu
Uzalendo...
Ningefahamu kitu chenyewe kinachokutatiza labda ningeweza kukufahamisha.

Nimeandika na nimezungumza kwenye video.

Wengi wameelewa.
 
Uzalendo...
Mimi nimeandika maisha ya Abdul Sykes kusahihisha historia ya uhuru wa Tanganyika.

Magaidi wa Msumbiji na hayo mengine yataingia vipi katika historia hii?

Hayo yanaandikwa kila siku na wataalamu wa mambo hayo.

Umesema kweli kuhusu Sykes.

Hakika nimewatafiti hasa na kwa undani mkubwa kiasi nimesababisha kuingizwa katika Cambridge Journal of African History (1998), Dictionary African Biography (2011) na majarida mengine mengi Ulaya na Marekani.

Hii imebadili historia nzima ya uhuru wa Tanganyika kama ilivyokuwa ikifahamika kabla.

Jonathan Glassman Mkuu wa Idara ya Historia ya Afrika, Northwestern University, Evanston Chicago, baada ya mimi kumzungumza hapo katika Ukumbi wa Eduardo Mondlane alisema kuwa hakika nimechangia pakubwa katika kuiweka sawa historia ya uhuru wa Tanganyika.

Kuwa nimefikia ukomo wa kujifunza umefanya haraka kuhukumu.

Nimeandika vitabu viwili 2020 na viko sokoni vyote vya historia.

Kimoja cha watoto wa shule za msingi kujifunza Kiingereza na Historia, "The School Trip to Zanzibar," na kingine "Rajabu Ibrahim Kirama," kinachoeleza vipi Uislam uliingia Uchaggani.

Screenshot_20211003-064810_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom