Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
ISSA SHIVJI NA ABDUL SYKES
Leo nilibahatika kukutana na Prof. Issa Shivji katika uzinduzi wa kitabu cha Abdilatif Abdulla, ‘’Voice of Agony.’’
Tulizungumza kidogo.
Nikakumbuka jinsi alivyomweleza Abdul Sykes katika kitabu chake, ‘’Law, State and the Working Class in Tanzania,’’ James Currey, London, 1986.
Miongo minne iliyopita kasoro kidogo.
Profesa Shivji katika kitabu hicho anamlaumu Abdul Sykes kwa kushirikiana na wakoloni na anamchukulia kama kabaila ambae yeye mwenyewe hatoki katika tabaka la wafanyakazi.
Aliandika haya akitafakari nafasi ya Abdulwahid kama kiongozi wa makuli katika bandari ya Dar es Salaam wakati wa ukoloni.
Shivji anasema:
"Serikali ilipenyeza uongozi wa makabaila katika Dar es Salaam Dockworkers Union."
Hapa Shivji alikuwa anaeleza jinsi Abdul Sykes alivyochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa kwanza katika historia ya vyama vya wafanyakazi Tanganyika mwaka wa 1947.
Bila shaka Prof. kwa kutoijua vyema historia ya maisha ya Abdul Sykes na vile vile kwa hamasa za misimamo ya mrengo wa kushoto ya Ki-Marx hasa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, Prof. akawa ametumia vipimo visivyo sawa katika kumchambua Abdul Sykes.
Wengi wanamkumbuka Abdul Sykes kwa mchango wake mkubwa kwa kumwezesha Mwalimu Nyerere kuchukua uongozi wa TANU uliopelekea Mwalimu kuwa kiongozi wa Tanganyika huru.
Nami nilipoandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes (1998) nikamweleza kama nilivyomfahamu.
Prof. Issa Shivji