Abdul Sykes wa leo ndani ya Historia ya TANU 1954

Abdul Sykes wa leo ndani ya Historia ya TANU 1954

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
ABDUL SYKES WA LEO 2021 NDANI YA HISTORIA YA TANU 1954

Kuna video ya Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Kilumbe Shaban Ng'enda anamtaja Abdul Sykes kama Mzee Abdul.

Video hii nimerushiwa na watu wengi niitazame.

Mh. Ng'enda anasema Mwalimu Nyerere alitwa na Mzee Abdul Sykes, "Wewe kijana umesoma..." yeye Abdul akiwa mzee na elimu hafifu anamwita kijana Julius Nyerere aje aongoze TAA.

Mheshimiwa hakupata kumjua Abdul Sykes wala kuijua historia ya TANU.

Katika hili hatulaumiani wengi tuko kizani na ndiyo sababu ya makosa katika yale aliyosema Mh. Ng,enda.

Ng'enda kiongozi wa CCM haijui historia ya TANU.

Wasikilizaji wanachama wa CCM halikadhalika hawaijui historia ya TANU.

Kwanza Abdul Sykes hakuwa mzee wakati anakutana na Nyerere mwaka wa 1952 wala katika umri wake hakufikia uzee.

Abdul Sykes amefariki akiwa na miaka 44.

Abdul alikuwa na miaka 28 na Nyerere alikuwa na miaka 30 pale walipofahamiana mwaka wa 1952.

Hili la kwanza.

Pili hakuna mtu yeyote aliyemwita Nyerere katika TAA ili achukue uongozi.

Nyerere alikuwa mwanachama wa African Association Tabora toka mwaka wa 1946 na alikuja Dar es Salaam akiwa mwanachama.

Alipomuuliza Kasella Bantu habari za TAA akiwa Pugu anasomesha ndipo Kasella Bantu akampeleka nyumbani kwa Abdul Sykes ambae alikuwa Kaimu Rais wa TAA na Katibu.

Angalia picha ya Abdul Sykes na Julius Nyerere 1957 Abdul ana miaka 33 na Nyerere miaka 35.

Screenshot_20210711-150542_WhatsApp.jpg
 
Same ol' shit from geezer who never ever ever ever quits peddling same ol' fuckin' shit even if it takes 200 years to force his shit down people's throats
 
Ahsante kwa ufafanuzi...
Smart...
Ni muhimu kwangu kusahihisha historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kwa sababu hii ni historia ya wazee wangu ningependa sana ielezwe kwa ukweli wake.

Najua sana kuna watu wanaghadhibika na wao wangependa tubakie na historia rasmi iliyomtoa Abdul Sykes lakini vipi utamfuta Abdul mtu aliyetaka kuunda TANU mwaka wa 1951 kwa kumleta Chief David Kidaha Makwaia katika TAA kama President?

Vipi utamfuta Abdul Sykes, Hamza Mwapachu na wazalendo wengine kama Dr. Kyaruzi na Dr. Michael Lugazia waliokuwapo TAA HQ, New Street wakati mipango inapangwa ya kuelekeza nguvu UNO 1950?

Wewe hujiulizi vipi iwe kadi no 1 ya TANU ni Julius Nyerere, no 2 Ally Sykes no 3 Abdulwahid Sykes no. 7 Abbas Sykes?

Hii iko vipi?

Halafu Chuo Cha Kivukoni CCM wanaandika kitabu cha historia ya TANU hawa ndugu watatu ambao baba yao ni muasisi wa African Association na ndiyo waliokuwa bega kwa bega na Nyerere hawatajwi kitabuni?

Ndugu yangu Smart huoni kama hili linastaajabisha?
 
Smart...
Nimekuuliza swali.
Huoni kuwa ni ajabu?
Mambo mengi kwenye historia haswa waasisi na wapigania uhuru yamefichwa fichwa sana...

Tunaaminishwa mambo mengine ambayo ndivyo sivyo...

Mfano Bibi Titi mohmmed sehemu nyingi tu anatajwa kwa ufupi sana au hatajwi kabisa...
 
Smart...
Soma hapo chini:

TATIZO KATIKA UTAFITI NA UANDISHI WA HISTORIA YA TANU1962

May 26
UTANGULIZI

Msomaji wangu jina lake Madagascar baada ya kusoma moja ya makala zangu niliyoeleza kuwa mradi wa kwanza wa kuandika historia ya TANU ulikuwa mwaka wa 1962 watafiti na waandishi wakiwa Abdul Sykes na Dr. Wilbert Klerruu.

Nilieleza kuwa Abdul Sykes alijitoa katika utafiti ule na Dr. Klerruu akabakia peke yake kukamilisha kazi.

Huyu msomaji wangu jina lake Madagascar aliniandikia kutaka kujua sababu ya Abdul Sykes kujitoa.

Nikamweleza huyu msomaji wangu maneno hayo hapo chini:

Madagascar,
Kleruu alikuwa hana moja alijualo katika historia ya AA.

Abdul Sykes kwanza alikuwa na mswada wa kitabu alioandika baba yake.

Mswada huu ulikuwa kumbukumbu za baba yake akieleza historia ya vipi babu yake Sykes Mbuwane alikuja Germany Ostafrika 1800 mwishoni kama askari mamluki chini ya Hermann Von Wissman.

Ndani ya mswada huu Kleist Sykes anaeleza maisha yake chini ya utawala wa Wajerumani hadi WW I akiwa askari ndani ya jeshi la Kamanda Paul Von Lettow Vorbeck.

Anaendelea kueleza utawala wa Waingereza baada ya WW I 1918.

Anaeleza alivyounda African Association 1929 baada ya kukutana na Dr. Kweggiyr Aggrey 1924.

Anaendelea kueleza kilichomsukuma kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) pamoja na Mzee bin Sudi na Ali Jumbe Kiro1933 kikiwa chama pembeni ya AA.

Hawa wazee wote ni babu zangu na koo hizi bado zipo Dar es Salaam mpaka leo.

Hapa katika miaka ya 1930s anaeleza juhudi za Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika kujenga shule ili Waislam kama Wamishionari wawe na shule zao akiweka msisitizo wa Qur'an kusomeshwa kama somo katika shule.

Kleist anaeleza ushawishi wa Waislam katika taasisi hizi mbili AA na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na nguvu iliyozuka katika kukabiliana na ukoloni.

Ile nguvu ya Uislam na Waislam ndani ya TANU inatokana na historia hii.

Bahati mbayo wapo wasiopendezwa na historia hii lakini huu ndiyo ukweli.

Abdul haya licha ya kuwa yameandikwa na baba yake lakini kazaliwa na kukua ndani ya historia hii.

Baada ya WWII na akiwa askari wa KAR ndani ya Burma Infantry akawa anaandika vipi vita hivi vilivyowasaidia Waafrika kujitambua na kuamua kudai uhuru wa Tanganyika.

Yeye binafsi alikuwa na mchango wake katika kuwakabili Waingereza kwanza kupitia Dockworkers Union akiwa Secretary General 1948 kisha haada ya kuchukua uongozi wa TAA 1950 akiwa TAA Secretary na Dr. Vedasto Kyaruzi President.

Kipindi hiki ndicho kipindi muhimu sana katika historia ya TAA kwani vijana wengi kutoka Makerere College walijiunga na TAA mjini Dar-es-Salaam pale New Street.

Hiki ndicho kipindi cha bongo za kizazi kipya cha wakati ule akina Hamza Mwapachu na viongozi wengine kutoka Kanda ya Ziwa kama Ali Migeyo, Saadan Abdu Kandoro na Paul Bomani wakaanza kukusanya nguvu zao pamoja kumkabili Gavana Edward Francis Twining.

Abdul na Hamza Mwapachu wanaweka msingi wa kuunda TANU na kutafuta kiongozi mmoja kuongoza harakati za uhuru.

Abdul yeye alimtaka Chief David Kidaha Makwaia ndiye aje TAA waunde TANU.

Mwapachu yeye mtu wake alikuwa Julius Nyerere lakini mwaka wa 1950 Nyerere alikuwa hajulikani wakati Chief Kidaha alikuwa maarufu na mjumbe wa LEGCO toka mwaka wa 1945.

Abdul Sykes 1950 tayari alikuwa halikadhalika kijana maarufu, kiongozi wa TAA na alikuwa mjumbe katika TAA Political Subcommitee pamoja na Mwapachu, Kyaruzi, Sheikh Hassan bin Ameir na Steven Mhando kwa kawataja wachache.

Huu ndiyo mwaka Abdul Sykes alikwenda Nairobi kufanya mazungumzo na Jomo Kenyatta agenda ikiwa Tanganyika na Kenya kuunganisha nguvu zao kukabiliana na Mwingereza.

Hii kamati niliyoitaja hapo juu TAA Political Subcommittee ndani yake alikuwapo Mwanasheria Earle Seaton akitoa ushauri nyuma ya pazia.

Huyu Earle Seaton alikuwa rafiki ya Abdul Sykes na wote wawili walikuwa rafiki wa Paramount Chief Thomas Marealle.

Hii ndiyo kamati akiwemo Dossa Aziz na John Rupia iliyokuja kuunda chama cha TANU 1954.

Lakini muhimu katika yale aliyoandika Abdul Sykes ni kueleza mkutano nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio, Ukerewe alipokwenda kaongozana na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Agenda kuu ya kikao hiki nyumbani kwa kwa Mwapachu ilikuwa kupata kauli ya yake kuhusu kumtia Nyerere kwenye uongozi wa juu kabisa wa TAA.

Hamza alimshauri Abdul kuwa Nyerere asaidiwe ashinde uchaguzi wa 1953 awe President na 1954 TANU iundwe.

Haya kwa kifupi ndiyo Abdul Syked aliyoandika katika kueleza chimbuko la TANU na Abdul akaeleza vipi alikuja kujuana na Nyerere 1952.

Inasemekana kuwa Julius Nyerere hakupendezewa na historia hii.
Abdul akajitoa katika ule mradi akamwacha Dr. Kleruu.

Naweka kitabu cha Abubakar Ulotu, ‘‘Historia ya TANU,’’ kitabu kilichotokana na utafiti na uandishi wa Dr. Wilbert Klerruu.

Hiki kitabu cha Abubakar Ulotu ni kutoka mswada wa historia ya TANU kilichokuwa kinaandikwa pale TANU Office na Abdul Sykes na Dr. Wilbard Kleruu mwaka wa 1962.

Historia hii ya ukweli inawachoma wengi na huwapandisha ghadhabu kiasi cha kunitukana matusi makubwa.

Kosa langu likiwa kuandika historia ya wazee wangu.

Kama nilivyoeleza hapo juu Abdul Sykes alijitoa katika uandishi wa historia ya TANU.

Dr. Kleruu akaendelea na uandishi hadi ukakamilika lakini TANU hawakuweza kukichapa kitabu kile.

Abubakar Ulotu akachukua mswada ule kwa siri na bila idhini ya TANU akachapa kitabu baada ya kufanya mabadiliko kidogo akaweka jina lake kama mwandishi.

Hivi sasa kipo kitabu cha maisha ya Julius Nyerere.

Muhimu kujua nini kimeandikwa kuhusu uasisi wa TANU na mchango wa Nyerere.

Waandishi wa kitabu hiki walifanya mahojiano na mwandishi kama picha zinavyoonyesha na walimtunuku nakala kwa mchango wake huo.

Fursa ikipatikana In Shaa Allah nitaeleza ninayohitilafiana na waandishi wa kitabu hicho kama nilivyo hitilafiana na kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni na kitabu cha Abubakar Ulotu.

1626264112174.png

1626264181330.png

1626264358084.png

1626265164944.png

Mswada wa Kleist Sykes kama ulivyoandikwa na mjukuu wake Aisha ''Daisy'' Sykes ni moja ya sura, ''Kleist Sykes The Townsman,'' ndani ya kitabu hicho hapo juu, ''Modern Tanzanians'' (1973) kilichohaririwa na John Iliffe.
 
Same ol' shit from geezer who never ever ever ever quits peddling same ol' fuckin' shit even if it takes 200 years to force his

Mambo mengi kwenye historia haswa waasisi na wapigania uhuru yamefichwa fichwa sana...

Tunaaminishwa mambo mengine ambayo ndivyo sivyo...

Mfano Bibi Titi mohmmed sehemu nyingi tu anatajwa kwa ufupi sana au hatajwi kabisa...
Smart...
Angalia wapi alipotokea Bi. Titi:

 
Back
Top Bottom