Msongoru
JF-Expert Member
- Apr 16, 2008
- 306
- 24
Na Juliet Kulangwa
Waswahili wanasema mguu wa kutoka mtume kaubariki na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Abdulhalim Hafidh Salim ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alijinyakulia kitita cha shilingi za Tanzania Milioni 10.
Mbali na kujishindia pesa hiyo katika shindano la Maisha Plus anakuwa Mtanzania wa kwanza kuibuka kidedea katika mashindano yaliyowahi kufanyika nchini akiwakilisha pande za Visiwani.
Kubwa kuliko zote ni kwamba wakati akikabidhiwa ushindi na pesa Tanzania ilikuwa ikitimiza miaka 45 ya muungano wake....Miasha Plus nayo iliwaunganisha kimtindo.
Mwananchi ndiyo gazeti la kwanza nchini lililopata nafasi ya kwanza ya kufanya mahojiano 'exclusive' na mshindi huyu........ kama hutaki haya lakini habari ndiyo.
Starehe- Unajisiakiaje kuwa mshindi katika shindano hili?
Abdul- Kila mmoja alikuwa na ndoto ya kuibuka kidedea, lakini kubwa kuliko zote nolifurahi sana kwa kuwa ushindi unamaanisha pia niliweza kushinda kila jaribio lililokuwapo ndani ya kijiji.
Kula maharage kila siku, kukata kuni, kupika, kuosha vyombo, task za hatari na mambo mengine ndio yalikuwa maisha yetu ya kila siku, kushinda yote haya ndiyo kushinda milioni kumi. Nimefurahi kwa kuwa lengo langu la kwanza limetimia.
Starehe- Kwanini unasema lengo lako la kwanza limetimia
Abdul- Lengo la kwanza lilikuwa ni kushinda na kutwaa milioni kumi lakini hiyo milioni kumi ina mipango yake ambayo pia inahitaji kuyafikia.
Starehe- Ni malengo gani hayo
Abdul- Its too soon to tell
Starehe-Wewe ni mmoja kati ya washiriki waliokuwa vinara katika shindano hilo tangu mwanzo kabisa, kuna siri yoyote ya ushidni wako.
Abdul- Nilikuwa na kontena la vituko na kwa bahati mbaya shindano limeisha nikiwa nimetumia robo tuu ya vituko vyangu......lakini kura moja ya Mtanzania ndiyo imenisimisha hapa naiheshimu sana.
Starehe- Umejifunza nini katika kijiji cha Maisha Plus.
Abdul- Nimejifunza mambo mengi lakini kubwa zaidi ni kuishi na watu kutoka sehemu tofauti,
Starehe- Upendo, mshiriki kutoka Mwanza aliwahi kusema kuwa wewe ndiye uliyeiweka ile hirizi ****** , je ni kweli ilikuwa ya kwako na kama sio uliipokeaje tuhuma zile.
Abdul- Kila kilichokuwa kikitokea kwenye kijiji cha Maisha Plus kilikuwa kinareflect maisha yetu ya huku majumbani mwetu, iliniuma kwa kuwa nilikuwa siwezi kuprove kuwa sihusiki katika lile, lakini nililipokea na kulichukulia kama changamoto katika maisha ya kila siku na niliweza kulishinda.
Starehe- Unauzungumziaje ushindi wako
Abdul- Baada ya Mungu na wazazi wangu nawashukuru sana Watanzania kwa kunipigania, siwezi kugawana nao hii zawadi lakini wajue ushindi wangu ni wa kwao, ile kura waliyopiga imewapa ushindi, nawashukuru sana na nina waombea mema kila siku.
Starehe- Unaushauri wowote kwa Rais
Abdul- Kwanza naomba aitambue Maisha Plus....hii ni zaidi ya taasisi ya elimu. Watanzania ni mashahidi wanaweza kunisaidia katika hili. Pili atimize ahadi alizotoa kwenye kampeni zake mwaka 2005.
Abdul alizaliwa miaka 25 iliyopita huko kwenye kisiwa cha marashi ya karafuu, ni mhitimu wa shule ya sekondari Vikokotoni .........ushanifahamu