Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Abdulghafar Idrisa Juma, Mbunge wa Jimbo la Mtoni
Mhe. Abdulghafar Idrisa Juma, Mbunge wa Jimbo la Mtoni tarehe 04 Mei, 2023 alipata nafasi ya kuchangia suala la Tanga Cement na Twiga Cement wakati wa kuwasilishwa kwa hoja ya bajeti ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara iliyosomwa na Waziri mwenye dhamana Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
"Sheria inasema wazi kwamba kampuni zikitaka kuungana na kuingia sokoni haitakiwi kuzidi asilimia 35 ya hisa, Tume ya Ushindani wa Kibiashara na Haki (FCC) ambao wana dhamana na mamlaka ya kusimamia sheria ya ushindani na jambo hili (mchakato wa Tanga Cement kununuliwa na Twiga Cement) walikiri kwa kusema kwamba kampuni hizi zisiungane kwa kuwa watazidi 35%, je ni kitu gani ambacho kimetokea na kuwasahaulisha FCC yale waliyoyasema wao wenyewe (FCC) na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara na Haki (FCT)" - Mhe. Abdulghafar Idrisa Juma, Mbunge wa Jimbo la Mtoni.