Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mjukuu wa Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar amesoma historia ya TANU jinsi
ilivyoingia Jimbo la Kusini (Southern Province) kupitia juhudi za wazalendo kama
Suleiman Masudi Mnonji, Yusuf Chembera, Salum Mpunga na Bi. Shariffa bint
Mzee kwa kuwataja wachache.
Hii ikagonga fikra yake mara moja akaniandikia kunifahamisha kuwa na yeye ana
historia ya babu yake Abdulkarim Hajj Mussa Jamadar mmoja kati ya wazalendo
wa mwanzo kumuunga mkono Mwalimu Nyerere na kusaidia kuiingiza TANU Kilwa
Mtoni na akaniahidi kuniletea picha ya nyumba ambayo Mwalimu Nyerere alikuwa
akifikia kila alipokwenda Kilwa na picha ya pikipiki ambayo babu yake alikuwa
akimpakia Nyerere wakisafiri kwenda kijiji hadi kijiji kuwahamasisha wananchi waingie
TANU kupigania uhuru wa nchi yao.
Haukupita muda Abdulkarim akanitumia picha ya pikipiki ya babu yake ambayo ndiyo
ulikuwa usafiri wao yeye na Nyerere kuvifikia vijiji vya jirani wakati wa kueneza TANU.
Pamoja na picha ya pikipiki akaniletea na picha ya nyumba ya babu yake ambayo
Mwalimu Nyerere alikuwa akifikia na vilevile picha ya nyumba ya Mwinyi Mcheni Omari
ambayo ndipo ikifanyika mikutano ya ndani ya TANU,
Nimemsihi Abdulkarim awasiliane na Makumbusho ya Taifa ili pikipiki hii iwekwe pale kwa
ajili ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa katika harakati zake za kudai uhuru.
Hii pikipiki ilihamishwa na mtoto wa Mzee Abdulkarim, Mohamed Abdulkarim na kupelekwa
Mafia Kilindoni.