CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amesisitiza umuhimu wa kudumisha umoja, mshikamano na ushirikiano baina ya watanzania wote bila kujali dini, kabila wala rangi kwa kuwa ni suala la Kikatiba na msingi wa ubinadamu.
Kinana ametoa ujumbe huo wakati akifungua tamasha la siku tatu la Shree Goverdhannathji Haveli kwa ajili ya kuonyesha maisha ya Kiimani, mafundisho Krishna ambayo yamewaleta pamoja jamii ya Kihindu kutoka Pande mbalimbali za Tanzania Na nchi ZA jirani.
Makamu Mwenyekiti amesisitiza kwamba Katiba y Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania inatoa fursa ya watu wote kuabudi Dini wanayoipenda na kufanya shughuli zao bila kubugudhiwa Na kwamba Serikali yetu haina Dini. Hata hivyo aliwataka waumini Wa Dini mbalimbali kusimama katika misingi inayolenga kudumisha umoja na mshikamano kwa watu wote.