Abdulrahman Kinana asisitiza umoja, amani na mshikamano kwa Taifa

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amesisitiza umuhimu wa kudumisha umoja, mshikamano na ushirikiano baina ya watanzania wote bila kujali dini, kabila wala rangi kwa kuwa ni suala la Kikatiba na msingi wa ubinadamu.

Kinana ametoa ujumbe huo wakati akifungua tamasha la siku tatu la Shree Goverdhannathji Haveli kwa ajili ya kuonyesha maisha ya Kiimani, mafundisho Krishna ambayo yamewaleta pamoja jamii ya Kihindu kutoka Pande mbalimbali za Tanzania Na nchi ZA jirani.

Makamu Mwenyekiti amesisitiza kwamba Katiba y Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania inatoa fursa ya watu wote kuabudi Dini wanayoipenda na kufanya shughuli zao bila kubugudhiwa Na kwamba Serikali yetu haina Dini. Hata hivyo aliwataka waumini Wa Dini mbalimbali kusimama katika misingi inayolenga kudumisha umoja na mshikamano kwa watu wote.
 
Waanze wao kwa kuacha ufisadi na watende haki
 
Kinana kama sio umri ndio alipashwa kuwa Rais wa JMT baada ya Samia
 
Kinana Jembe sana huyu mzee
 
aende kwao somalia akahamasishe amani watu waache kuchinjana. Hapa wanatuibia halafu wanataka sisi tudumishe amani, amani ipi? Amani ya taifa kuendelea kuwa masikini na wao mafisadi kujitajirisha? nehi nehi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…