Baba wa Taifa ni Nyerere. Wajumbe walimpiga Chini Sykes na kumchagua Nyerere.
Economist,
Umeghadhibika.
Hapana sababu ya maneno makali kama hii ''Kupiga chini.''
Hapakuwa na uadui katika kutafuta kiongozi wa TAA.
Abdul Sykes alikwenda Nansio, Ukerewe kwa Hamza Mwapachu akifuatana na Ali Mwinyi Tambwe, Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).
Abdul Sykes alikwenda kwa Hamza Mwapachu ili apate kauli yake ya mwisho kuhusu uchaguzi wa TAA wa mwaka wa 1953 na kumtia Nyerere katika uongozi.
Hii ni historia ndefu sana lakini kwa ufupi Nyerere aliingizwa katika uongozi kama Hamza Mwapachu alivyoagiza.
Soma hapo chini uongozi wa uliopitishwa wa uchaguzi ule:
Mwezi June, makao makuu ya TAA yalitangaza kamati yake ya utendaji: J. K. Nyerere, Rais, Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais; J. P. Kasella Bantu, Katibu Mkuu; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Katibu wa muhtasari; Wajumbe wa Kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko.
(Tanganyika Standard, 19 June, 1953).
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes (1998).
Sasa hii ''kupigwa chini'' ina maana gani?
Hakuna anaepinga kuwa Julius Nyerere ni Baba wa Taifa.
View: https://youtu.be/GR0DQyhAdHs