Hawatajwi ?, Mbona wewe umewataja ?
Kwa taarifa yako kuna mashujaa wa ukweli (unsung heroes) hata wasiofahamika...., Nadhani unajua msemo wa Avumae Papa Baharini.... Kwahio cha maana kila anayejua / anayemfahamu shujaa wake sio vibaya akamtaja, otherwise tutahitaji robo tatu ya historia ikitaja watu (ambayo sio mbaya) ila in summary nadhani matokeo ni muhimu zaidi na kutajana iwe subset
Key...
Kwangu mimi imesadifu kuwa wazee wangu ndiyo mashujaa wa wote kwa kuwa walipigania uhuru wa Tanganyika.
Hii ndiyo sababu kuu ya mimi kuandika historia yao ambayo haikuwa imehifadhiwa.
Ninao wajomba zangu na baba zangu ambao katika siku zilizopita hapa mjini Dar es Salaam walivuma kwa sifa kadhaa kama kucheza Gossage Cup na kukichukua kikombe.
Ninao ambao walikuwa hodari katika muziki na rekodi zao za santuri zilirekodiwa na Hugh Tracey, Mzungu kutoka Rhodesia zikatolewa santuri na Gallotone Johannesburg.
Lakini hawa hawakunivutia kama hawa waliounda AA 1929, Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika1933, Dockworkers Union 1948, TANU 1954 na Tanganyika Railways African Union.
Hata hivyo hii haiwakatazi wengine kuandika vitabu vya mashujaa wao.
Mimi nina jumla ya vitabu 10 nimeandika hadi sasa vya historia ya hawa wazee wangu.
Wengine nimeweza kuwatia katika Dictionary of African Biography (DAB), Oxford Univeristy Pressm New York (2011) (Volume 6) na yote haya ni yenye faida kwetu kama taifa na kwa vizazi vijavyo.
Hiyo picha ni Gossage Team Winners 1949 kuna wazee wangu watatu katika timu hiyo.
Salum Abdallah huyu ni babu yangu muasisi wa TANU Tabora, Western Province 1954 na Rais Muasisi wa TRAU 1955 ana historia kubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Vipi nitaacha kuandika historia ya hawa wazalendo?