Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hapo juu ni sehemu ya taarifa za Abdul Sykes kutoka kumbukumbu za Waingereza.
Nikisoma hii taarifa nimekutana na makosa mengi sana kuanzia majina yake, umri,
kabila yake hadi kazi alizofanya.
Sijui kwa nini iwe hivi.
Nimemuomba aliyenipatia hii nyaraka anipe, ''source,'' ingawa naamini hii ni taatifa
ya Special Branch:
(FCO 141/17808 at Kew, UK National Archives. from letter of Special Branch to the Chief Secretary, dated 17 April 1953. Discussion of 'Action Group', that were trying to take control of Tanganyika African Association in Dar.Letter had appendix called 'Notes on known members of the ACTION GROUP. That is where this entry on Abdulwahid comes from).
Lakini juu ya haya yote kuna habari katika hii nyaraka ambayo mimi kwa mara ya
kwanza alinieleza Ahmed Rashad.
Hii ni kuhusu mkutano wa siri aliofanya Abdul Sykes na Jomo Kenyatta Nairobi
mwaka wa 1950.
Nimeueleza mkutano huu kwa kirefu katika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.
Katika taarifa hiyo hapo juu kuna habari za Appa B. Pant.
Huyu alikuwa Balozi (High Commissioner) wa India Kenya.
Katika taarifa yake ya mwaka wa 1950 kwa wanachama wa TAA Abdul ameeleza
mazungumzo yake Nairobi na Bwana Pant.
Haya mazungumzo pia nimeyaeleza katika kitabu cha maisha yeke:
''Mwaka 1950, Abdulwahid alisafiri kwenda Nairobi kukutana na Jomo Kenyatta ili kuanzisha uhusiano na Kenya African Union (KAU).Abdulwahid alifunga safari hii wakati wa mashindano ya kandanda ya Kombe la Gossage. Haya yalikuwa mashindano ya kila mwaka ambayo nchi tatu za Afrika ya Mashariki pamoja na Zanzibar zilikuwa zikishiriki. Huenda Abdulwahid alichagua wakati huu mahsusi ili kuficha dhamiri ya safari yake. Kama mtu labda angetaka kujua sababu ya safari yake ingewezekana kwa urahisi kabisa kuelezwa kuwa alisafiri kwenda Nairobi kutazama mashindano ya Gossage. Abdulwahid alifikia Railway Hotel na alikwenda kuonana na Kenyatta usiku akifuatana na rafiki yake mpenzi kutoka Zanzibar, mmoja wa wacheza mpira katika timu ya Zanzibar. Abdulwahid na rafiki yake walikwenda nje kidogo ya Nairobi kwenye nyumba moja iliyokuwa imegubikwa na giza na kuzungukwa na walinzi wa Mau Mau. Abdulwahid alikuwa anatarajiwa. Kenyatta alipofahamishwa kuwa Abdulwahid amefika na yupo nje, alitoka kumlaki. Kenyatta alikuwa akimfahamu Ally Sykes tangu mwaka 1946. Inawezekana kuwa kazi ya Abdulwahid ilirahisishwa na uhusiano huu wa Kenyatta na mdogo wake. Mzanzibari huyu aliyemsindikiza Abdulwahid alikutana na Kenyatta na wakapeana mikono.
Baada ya kutambulishwa Kenyatta, Abdulwahid, Fred Kubai, Bildad Kaggia na Kungu Karumba waliingia kwenye chumba kingine ambako mkutano ulifanyika. Mzanzibari, rafiki yake Abdulwahid alibakia nje na mlinzi.''
HISTORIA YA JOMO KENYATTA NA ABDULWAHID SYKES 1950
Utangulizi Leo nilipokuwa nikipitia gazeti la Mwananchi (Jumanne Aprili 5, 2016) nilikuta kipande hicho hapo chini kuhusu Jomo Kenyatt...