Mdukuzi,
Halikadhalika babu yangu mkuu Samitungo Muyukwa aliingia Germany Ostafrika akitokea Belgian Congo akiwa askari katika jeshi la Wajerumani kuwasaidia kuitawala Tanganyika.
Kituo chake cha kwanza ilikuwa Boma la Shirati na ndipo alipozaliwa babu yangu.
Hakika hawa askari waliwasaliti ndugu zao Waafrika.
Hizi ndizo athar za ukoloni.
Lakini mtoto wake yaani babu yangu Salum Abdallah alisimama kupambana na ukoloni wa Waingereza akiwa mmoja wa wazalendo walioasisi TANU na kufanya mengi kwa maslahi ya nchi yake.
Na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mtoto wa Sykes Mbuwane Kleist.
Aliasisi AA chama kilichokuja kuunda TANU wanae watatu wakiwa waasisi wake na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mimi ni kizazi cha tatu cha Samitungo Muyukwa na mchango wangu ni kuwa nimeweza kutafiti na kuijua historia ya wazee wangu na kuiandika.
Leo tuko hapa tunaisoma na kuijadili.