Abdurahman Yunusu adaiwa kutekwa na watu wasiojulikana wakiwa na Land Cruiser Geita, majibu ya polisi hayaridhishi

Abdurahman Yunusu adaiwa kutekwa na watu wasiojulikana wakiwa na Land Cruiser Geita, majibu ya polisi hayaridhishi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Familia ya Mariamu Ibrahim Juma, mkazi wa Mtaa wa Uwanja, Kata ya Nyankumbu, Mjini Geita, imeiomba serikali kupitia Jeshi la Polisi kusaidia kumtafuta mtoto wao, Abdurahman Yunusu (24), ambaye ametoweka kwa siku 13 katika mazingira ya kutatanisha.

Akizungumza na Wasafi Media, mama mzazi wa kijana huyo, Mariam Ibrahim Juma, alisema mwanaye alichukuliwa na watu wasiojulikana kutoka dukani kwake alikokuwa akiuza bidhaa. Watu hao be walimuingiza kwenye gari aina ya Land Cruiser na kuondoka naye, na tangu Machi 1, 2025, hajulikani alipo.

"Tayari nimepita vituo vyote vya polisi hadi kwa RPC wa Geita, lakini majibu si ya kuridhisha. Naomba serikali inisaidie kumpata mwanangu, akiwa hai au hata kama amekufa," alisema kwa uchungu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi wa Polisi (SACP) Safia Jongo, amethibitisha kuwa watu wanne wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na kutoweka kwa kijana huyo. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi.

Soma Pia:

 
Maisha magumu kutekwa nako kuko pale pale polisi mtupumzishe bwana.
 
Back
Top Bottom