mwakani naolewa
Senior Member
- Jul 25, 2024
- 148
- 426
Abiria waliokua wakisafiri na treni ya TAZARA kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya wamepaza sauti zao kujua nini hatima ya safari yao baada ya kukaa stesheni ya treni Dar es salaam tangu jana septemba 3, wakisubiri kusafiri mpaka leo septemba 4, baada ya kupokea matangazo ya kuahirishwa kwa safari yao bila ufafanuzi wowote kutoka mamlaka husika na ofisi za viongozi wa stesheni zimefungwa.
Abiria waliokuwa wanasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya kwa treni ya TAZARA wamekwama kwenye stesheni ya TAZARA mkoani Dar es Salaam kuanzia saa nane mchana wa Septemba 3, 2024 huku wakipokea matangazo ya kuahirishwa kwa safari yao bila ufafanuzi wa sababu za kuahirishwa huko.
Abiria hao wameiambia Azam TV kuwa uongozi wa shirika la reli haujajitokeza kuwapa taarifa yoyote ya ziada.
Azam TV
TAZARA inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa abiria wote waliotakiwa kusafiri na Treni ya abiria ya Kilimanjaro kutoka stesheni ya Dar es Salaam siku ya Jumanne saa Saba na dakika Hamsini Mchana (13.50)
Hali hii imesababishwa na kuchelewa kuwasili kwa treni hiyo kutoka Mbeya. Kwa mujibu wa ratiba treni ya Kilimanjaro ilitakuwa kuwasili siku ya Jumapili tarehe 01.09.2024 saa kumi na moja na dakika ishirini Jioni (17:20) na kuondoka siku ya Jumanne tarehe 03.09.2024 saa saba na dakika Hamsini mchana (13:50), badala yake iliwasili siku ya Jumanne tarehe 03.09.2024 saa saba kamili mchana (13.00) katika stesheni Kuu ya Dar es Salaam.
Mabehewa ya treni hiyo ya abiria yalihitaji matengenezo kabla ya kuondoka ili kuhakikisha usalama wa abiria. Kazi ya matengenezo imemalizika leo, Jumanne asubuhi tarehe 04.09.2024 na treni hiyo iliondoka saa tano na nusu asubuhi (11:30) kuelekea Mbeya.
TAZARA INAOMBA RADHI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA
TANZANIA ZAMBIA RAILWAY AUTHORITY,
4.9.2024

=====
KUCHELEWA KUONDOKA KWA TRENI YA ABIRIA YA KILIMANJARO KATIKA STESHENI YA DAR ES SALAAM.