KERO Abiria tunapata usumbufu mkubwa daladala Dodoma kukatisha ruti na kufaulisha abiria, mamlaka dhibiti kero hii

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Bado kuna shida kubwa sana ya madereva wa daladala kugeuzia njiani na kufaulisha abiria kwenye gari nyingine.

Imekuwa kero na usumbufu mkubwa sana hasa kwa daladala zinazotokea Mipango kuelekea Mjini. Serikali husika itusaidie kuweka askari kwenye vituo mbalimbali maana kufaulisha abiria sio vyema inatufanya tukae tena kwenye gari nyingine na tusubiri mpaka ijae jambo ambalo linatuchelewesha makazini.

Pia nauli haieleweki ukitoa hela ya noti unakatwa na shilingi mia ya ziada yaani mfano ukitoa 1000 unarudishiwa 400 badala ya 500 hivyo tunalazimika kuchenji hela mapema usiku ili kupata nauli kamili(huo ni mfano halisi wa gari zinazotoka Mipango kwenda Mjini)
 
Hii tabia mbaya sana, huwa inatia hasira pale unatoka kwenye daladala uliyokuwa umekaa na kufaulishwa ambayo unaend kudaka bomba.
 
Bado kuna shida kubwa sana ya madereva wa daladala kugeuzia njiani na kufaulisha abiria kwenye gari nyingine

Imekuwa kero na usumbufu mkubwa sana hasa kwa daladala zinazotokea Mipango kuelekea Mjini. Serikali husika itusaidie kuweka askari kwenye vituo mbalimbali maana kufaulisha abiria sio vyema inatufanya tukae tena kwenye gari nyingine na tusubiri mpaka ijae jambo ambalo linatuchelewesha makazini.

Pia nauli haieleweki ukitoa hela ya noti unakatwa na shilingi mia ya ziada yaani mfano ukitoa 1000 unarudishiwa 400 badala ya 500 hivyo tunalazimika kuchenji hela mapema usiku ili kupata nauli kamili(huo ni mfano halisi wa gari zinazotoka Mipango kwenda Mjini)
Unaweza hata kusahau mzigo,maana akili imejipa nashuka mjini na gari hili nililopanda ghafla unabadilisha lingine! Noma hiyo konda na dereva wako.
 
Duh afadhali nilikua Dom wiki juzi nililiona Hilo. Unapanda gari kwenda mjini wanakufaulisha au wanakuacha kituo Cha mbali wakikwambia gari haifiki kituo Cha mwisho. Utaskia panda bajaji mpaka majengo ni buku tu
 
Nauli si ni 600? au hiyo njia nauli bado 500
 
Duh afadhali nilikua Dom wiki juzi nililiona Hilo. Unapanda gari kwenda mjini wanakufaulisha au wanakuacha kituo Cha mbali wakikwambia gari haifiki kituo Cha mwisho. Utaskia panda bajaji mpaka majengo ni buku tu
Uliachwa wapi ukaambiwa upande Bajaj hadi Majengo?

Daladala kutokea Mipango destination ni Nyerere square, pia unaweza kupelekwa hadi General(Hospital), suala la wao wakupeleke hadi majengo sidhani kama lipo
 
Nimetoa mfano ya kinachotokea.
Uliachwa wapi ukaambiwa upande Bajaj hadi Majengo?

Daladala kutokea Mipango destination ni Nyerere square, pia unaweza kupelekwa hadi General(Hospital), suala la wao wakupeleke hadi majengo sidhani kama lipo
metoa
 
Jamani hata huo mji mdogo tu (uliopewa jina JIJI kiubishi) umeanza kuwashinda! Sasa wanaweza kitu gani? Nakumbuka Dar es salaam ndiyo kuna vurugu za Bodaboda na Bajaji wanaojipangia nauli hovyo hovyo na kupita kwenye traffic lights taa ikiwaka nyekundu huku LATRA wamelala usingizi wa pono.

Hata hili tunahitaji wazungu na wachina waje kutuelekeza cha kufanya! Marehemu Kingunge alisema ukweli kuwa mmeishiwa pumzi. Dar es Salaam ni mahali pachafu sana kuanzia mnakoita ushuani mpaka Tandale.

Badilikeni basi!. Ule utaratibu wa kufanya usafi kila Jumamosi tulipowaambia ni nguvu ya soda si mlibisha. Sasa kiko wapi si pumzi imekata! Simamieni usafi mtaa kwa mtaa.

Nendeni Kigali mkajifunze namna ya kusimamia usafi wa miji na majiji pamoja na kuyapanga hata kama yamekwisha vurugika. Wapinzani wenu wakitangaza maandamano ndiyo mnaibuka na WAJEDA kufagia miji.

Mimi naamini mnafanya makusudi kwa sababu mnaweza ila nia ndiyo hamna. Achia uchaguzi huru muone watu serious na maisha ya wenzao mpate kujifunza!
 
Hapo kwenye kukatwa 100 ukitoa hela kubwa hata Dar ipo hiyo kasumba, me juzi kati hapa tuliwakiana na Konda na nikatishia kupiga simu polisi ingawa aligoma kunirudishia Mia yangu ila baada ya kushuka niliona wanageuza ruti na kuwafaulisha abilia kwenye Gari lingine walihofia huenda nimekopy plate namba.

Wananchi wa Wadodoma msiwe wanyonge hao makonda wanapenda kuwakiwa msipowawakia wanawapanda kichwani.

Kuna daladala niliwahi kupanda lilikuwa linaenda Makumbusho lilitoka Mbezi, kawaida si lazima lipitie mawasiliano then lipakie au lishushe, sasa tulipofika pale mawasiliano konda na Dereva wake wakataka kubadili ruti yaani walitaka kugeuza kurudi mbezi kisa abiria walikuwa wachache kulinganisha na waliopanda aisee kuna jamaa alimuwakia Dereva na akatishia kuwapigia LATRA Simu Dereva aliogopa mwenyewe akajikuta anasema basi Baba wa sheria Acha tuwapeleke...

Kwahiyo wakati mwingine Mabadiliko huanza na wewe Mwanamchi wanasiasa hawawezi kukusaidia ukiangalia wao ndiyo wamilki wa hayo madaladala tumia Democrasia mkuu...
 
Bado kuna shida kubwa sana ya madereva wa daladala kugeuzia njiani na kufaulisha abiria kwenye gari nyingine.

Imekuwa kero na usumbufu mkubwa sana hasa kwa daladala zinazotokea Mipango kuelekea Mjini. Serikali husika itusaidie kuweka askari kwenye vituo mbalimbali maana kufaulisha abiria sio vyema inatufanya tukae tena kwenye gari nyingine na tusubiri mpaka ijae jambo ambalo linatuchelewesha makazini.

Pia nauli haieleweki ukitoa hela ya noti unakatwa na shilingi mia ya ziada yaani mfano ukitoa 1000 unarudishiwa 400 badala ya 500 hivyo tunalazimika kuchenji hela mapema usiku ili kupata nauli kamili(huo ni mfano halisi wa gari zinazotoka Mipango kwenda Mjini)
We bwana sio mpanda dala dala hata nauli haujui kua ni 600 saiv
 
Back
Top Bottom