SoC04 Abiria wa bodaboda wawajibike kulipa faini ya kutovaa helmet kama wanavyowajibishwa madereva

SoC04 Abiria wa bodaboda wawajibike kulipa faini ya kutovaa helmet kama wanavyowajibishwa madereva

Tanzania Tuitakayo competition threads

Lumbi9

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2014
Posts
8,666
Reaction score
12,178
Katika kuangalia usawa na udhibiti kwa ndugu zetu wanaoendesha vyombo vya moto vya pikipiki maarufu bodaboda nimeona tatizo halipo kwa madereva tu bali hata kwa abiria wao, mfano unakuta abiria anataka usafiri anapewa helmet ajikinge ama kupunguza madhara ya ajali endapo ikitokea abiria huyu utakuta anakataa kuvaa kwa makusudi kabisa au mwingine anaichukua na kuipakata miguuni, ikitokea wamekutana na askari wa usalama barabarani wakisimama lawama na faini zote zitamuendea dereva huyo wa bodaboda hali ya kuwa abiria alikataa kwa makusudi kabisa huku helmet ikiwepo pengine kaishikilia yeye mwenyewe, ndipo nikafikiria kwanini abiria huyu asiwe mtu wa kwanza kabisa kuwajibishwa na vyombo vya sheria kwa kutokuvaa helmet ambayo inaweza kumkinga ama kupunguza madhara mbalimbali ya ajali ikiwa itatokea, kukiwa na namna ya kuwajibishwa kwa abiria kwa usawa kama anavyowajibishwa dereva nafikiri hata abiria wataogopa kupanda hivyo vyombo bila kuvaa hizo kofia ngumu na kama bodaboda hana kofia ngumu ya ziada nafikiri hakuna abiria atataka kupanda bodaboda aina hiyo.

Yote kwa yote ni wajibu wa kila mtu kuhahikikisha usalama wake awapo barabarani bila kushurutishwa na vyombo vya usalama, yatupasa kushirikiana na watu wa usalama kuhakikisha madhara yanayoweza kuzuilika yanazuilika.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom