abiria wa pikipiki wana matatizo gani?

abiria wa pikipiki wana matatizo gani?

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Posts
1,508
Reaction score
220
huwa inanipa taabu sana, eti kwa nini abiria wa pikipiki huwa wanakaa "upande" kila mara huku wakichingulia "kiaina" juu ya bega la dereva.... yaani hawakai wima na kutazama visogo vya madereva wao?
 
Wanaokaa upande ni wanawake/wasichana. Nguo nyingine huwezi tanua miguu, na unaweza anguka wakati wa kupanda au kushuka. So, kukaa upande ni nafuu zaidi.
 
...khekhekhe, eti abiria na mkao wa "upande upande" huku anachungulia "kiaina"
ha ha ha...

Utawaumiza vichwa hapa kwenye jukwaa la mahusiano... :A S-coffee:
 
Wanaokaa upande ni wanawake/wasichana. Nguo nyingine huwezi tanua miguu, na unaweza anguka wakati wa kupanda au kushuka. So, kukaa upande ni nafuu zaidi.

...duhhh, haya bana. :tape:
 
Wanaokaa upande ni wanawake/wasichana. Nguo nyingine huwezi tanua miguu, na unaweza anguka wakati wa kupanda au kushuka. So, kukaa upande ni nafuu zaidi.
Nafikiri hujamuelewa mtoa mada. yeye anajaribu kuongelea wale wanaokaa huku kila mguu ukiwa upande mmoja wa pikipiki, hawa ukiwaangalia mara nyingi sana kama sio zote vichwa vyao huwa haviko usawa wa kichwa cha dereva yaani vinakuwa kushoto au kulia kwake kdogo huku wakichungulia mbele. Hao ndo anaowazungumzia mkuu.
 
sasa hapo kuna tatizo gani mtu akichungulia ili aone anapoenda sasa unataka aangalie kisogo bila kujua anapoenda au kuna hatari gani mbele

halafu hii mada mbona kama hapa sio sehemu yake?
 
Wanakwepa harufu ya kikwapa ya dereva............................
 
huwa inanipa taabu sana, eti kwa nini abiria wa pikipiki huwa wanakaa "upande" kila mara huku wakichingulia "kiaina" juu ya bega la dereva.... yaani hawakai wima na kutazama visogo vya madereva wao?

Kama tungo hizo sio tata basi hapa si sehemu ya kuijadili...
Haihusiani na mahusiano, urafiki wala makopa
 
Mi naona kama huwa wanakuwa na ka hofu flani ndo maana wanakaa upande kwa kujiandaa kwa lolote la mbele.
Alafu kwa nn wengine huwa wanakumbatia sana kwa dereva mpaka wanamkaba tumbo anapumua kwa tabu?
 
Back
Top Bottom