Abiria wa treni Dar - Moshi walalamikia ukatishaji tiketi wadai foleni ni ndefu sana

Abiria wa treni Dar - Moshi walalamikia ukatishaji tiketi wadai foleni ni ndefu sana

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Abiria wa treni ya Dsm kwenda Moshi wamemuomba mkurugenzi wa TRC ndugu Kadogosa kuwaboreshea Huduma za ukataji tiketi kwani abiria ni wengi na foleni ni ndefu sana.

Abiria hao wamedai kipindi hiki shule zimefungwa na wananchi wengine wanaenda nyumbani kula sikukuu za mwisho wa mwaka na treni hiyo ndio tegemeo lao.Wameomba TRC iweke utaratibu rafiki wa kukata tiketi katika kituo cha Kamata.

Chanzo: TBC

Maendeleo hayana vyama!
 
Abiria wa treni ya Dsm kwenda Moshi wamemuomba mkurugenzi wa TRC ndugu Kadogosa kuwaboreshea Huduma za ukataji tiketi kwani abiria ni wengi na foleni ni ndefu sana.

Hiyo management ina akili ya tope, wanashindwaje ku digitize!? Kama wameweza kuboresha reli wanashindwaje kuweka mfumo wa e-ticketing? Labda wana mitego yao ya kuiibia serikali kupitia manual system!!
 
Umenena vema!
 
TRC wajiongeze watumie e_ ticketing na wananchi watumie simu za mkononi kununua tickets zao Kama wanavyonunua luku. Bila e_ ticketing serikali itaibiwa pesa nyingi sana kipindi hili smbacho abiria ni wengi sana.
 
naskia huko kwenye treni watu ni kulewa mwanzo-mwisho
 
Unafungua huduna kwa style ile ile ya mwaka 1990... 29 yrs ago...watu wakisema wanaonekana eti wasaliti wa maendeleo...sasa haya ndiyo maendeleo? kufanya mambo kwa same style as it was 30 yrs back.

CCM juuuu...... chamaaa.!!
 
Ccm juu chama chetu kimeleta mapinduzi Tanzania jembe na nyundo......Hakyanani ujima hauishi nchi hii
Unafungua huduna kwa style ile ile ya mwaka 1990... 29 yrs ago...watu wakisema wanaonekana eti wasaliti wa maendeleo...sasa haya ndiyo maendeleo? kufanya mambo kwa same style as it was 30 yrs back.

CCM juuuu...... chamaaa.!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom