Abishai: Shujaa wa Daudi aliyesahaulika

PutinV

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2017
Posts
1,046
Reaction score
1,643


Abishai alikuwa mtoto wa Seruya dada yake Daudi. Pia alikuwa kaka wa Yoabu na Asaheli. Abishai ni moja kati ya wale mashujaa watatu ambao walikuwa mashuhuri kuliko wale thelathini.

Katika Biblia, Abishai anatajwa kwa mara ya kwanza katika 1 Sam: 26 ambapo Daudi akiwa katika mbuga za Zifu aliwauliza Ahimeleki Mhiti na Abishai kuwa ni nani ambaye yuko tayari kujitolea kushuka naye usiku katika kambi ya Shauli wakati ambapo adui wote watakuwa wamelala. Bila kusita Abishai alijitokeza kwenda pamoja na Daudi katika kambi ya adui, jambo ambalo lilikuwa ni hatari kwa maisha yao kwani ilifahamika kabisa kuwa wakati huo Shauli alikuja Zifu kwa makusudi mazima ya kumuua Daudi.

Baada ya kuingia katika kambi ya Shauli walipenya katikati ya jeshi zima hadi walipofika sehemu ambapo Shauli alikwa amelala jirani ya kamanda wake Abneri. Abishai alimuomba Daudi ruhusa ya kumpiga Shauli kwa pigo moja na asiamke tena. Kama wangefanya hivyo ingekuwa ni ushindi mkubwa kwa kambi ya Daudi lakini Daudi hakumruhusu kwani hakuona kuwa ni sahihi kumuua Masiha wa Bwana.



Wakati wa vita dhidi ya Waamori na Waashuru ilimbidi Yoabu kugawa jeshi lake mara mbili huku nusu ya jeshi likawa chini ya Yoabu ambaye alipigana na Waashuru na nusu nyingine chini ya Abishai ambaye alipigana na Waamoni hadi pale walipo pata ushindi mkubwa kwa Israeli.

Wakati Daudi alipokuwa mfalme juu ya Israeli, alipinduliwa na mwanawe Absalom na wakati akiwa njiani Bahurimu, akatokea Shimei mtu wa ukoo wa Shauli akaanza kumtukana Daudi na kumrushia mawe. Kile kitendo kilimuudhi Abishai ambaye alitaka kwenda kumshambulia Shimei lakini alikosa ruhusa ya Daudi.



Wakati wa vita dhidi ya majeshi ya Absalom Abishai aliongoza theluthi moja ya jeshi la Daudi huku theluthi mbili nyingine zikiongozwa na Yoabu na Ittai. Abishai na wenzake walimkatalia Daudi asijiunge nao katika vita kwani ingekuwa hatari kwake.

Wakati ambapo vita vilikuwa vimeisha na watu wa Daudi wamepata ushindi dhidi ya watu wa Absalom, Daudi alirudi Yerusalemu huku akiwa amesahau yote lakini Abishai hakusahau kitendo cha Shimei alipo mtukana Mfalme hivyo kwa mara nyingine alileta wazo la kumuua Shimei lakini Daudi alikataa kwa mara nyingine.

Wakati Daudi akiwa mfalme ulizuka uasi ambao uliongozwa na Sheba mwana wa Bikri ambapo Amasa alitumwa kwenda kukusanya jeshi zima la Israel lakini alishindwa kufanya hivyo kwa muda ulio pangwa. Kutokana na mahusiano duni kati ya Daudi na Yoabu kwa wakati huo, Daudi alimuamuru abishai akusanye jeshi la Israel lakini Abishai kwa kutokupenda makuu au kwa kumuogopa kaka yake Yoabu au kwa heshima kwa kaka yake alitoa madaraka kwa Yoabu ya kukusanya jeshi tofauti na mfalme alivyo elekeza. Abishai alishuhudia mauaji ya Amasa mwana wa Yetheri huko Gibeoni yaliyofanywa na kaka yake.

Wakati wa utawala wa Daudi kama mfalme kulikuwa na vita vya mara kwa mara dhidi ya Wafilisti ambapo Daudi mwenyewe alipigana vita hivi hata pale alipo kuwa mzee. Katika vita fulani dhidi ya Wafilisti Daudi alizimia wakati akipigana na jitu la Kifilisti, Ishbi-benonu lenye mkuki wenye ncha yenye uzito wa kilo tatu na nusu alizimia, lakini kabla halijammalizia Daudi, Abishai aliingilia na kumuokoa Daudi. Huo ulikuwa ni mwisho wa Daudi kwenda vitani na watu wake.



Abishai anatajwa katika mashujaa thelathini wa Daudi, alikuwa kamanda wa mashujaa wote thelathini wa Daudi. Abishai anasifika kwa uwezo wake wa kutumia mkuki, alipigana na watu mia tatu kwa kutumia mkuki wake na akashinda. Lakini jambo linalo shangaza ni kuwa Yoabu pamoja na uwezo wake kama kamanda na mambo yote hatajwi kama ilivyo kwa kaka yake Abishai ambaye anatajwa.

Daudi aliona kama wana wa Seruya ni watu wakatili wenye nia ya kumwaga damu na hii inaonekana kwa Yoabu na Abishai nduguye bila kusahau ndugu Yao Asaheli ambaye alikufa wakati anamkimbiza Kamanda wa Shauli yaani Abneri.

Lakini kuna tofauti kubwa kati ya Abishai na ndugu zake. Abishai tofauti na kaka yake Yoabu alimtii mfalme, tazama alivyo tii amri ya kutomuua Shauli, lakini hakika kama Yoabu angekuwepo eneo lile asingeondoka bila kumuua Shauli na Abneri lakini kwa utiifu Abishai alisikia amri ya mfalme na kumuacha Shauli aishi. Hivyo hivyo kwa Shimei.

Abishai hakupenda makuu kama kaka yake Yoabu ambaye hakutaka mtu yeyote juu yake katika masuala ya jeshi, ndio maana Amasa alipo shindwa jukumu la kukusanya jeshi, Daudi alimpa jukumu hilo Abishai naye abishai kwa kutambua uwezo wa Yoabu kijeshi hakumuacha Yoabu nyuma na walifanikiwa lakini walimwaga damu ya ndugu yao Amasa.

Kubwa kuliko yote ni mapenzi makubwa aliyokuwa nayo Abishai kwa mfalme Daudi. Sidhani kama kuna mtu aliyempenda Daudi kama Yonathani mwana wa Shauli, swali linakuja nani baada ya Yonathani?, si mwingine ni Abishai, jinsi alivyo hatarisha maisha yake na kushuka kambini kwa Shauli, jinsi alivyo umia wakati Shimei alipomtukana Daudi.

Wakati wa vita dhidi ya Wafilisti, Daudi alitamani kunywa maji katika kisima kilichokuwa huko Bethlehemu lakini kikwazo kilikuwa ni jeshi la Wafilisti lilokuwa katikati yao. Mashujaa watatu miongoni mwa watu wa Daudi walishuka hadi Bethlehemu wakipita katikati ya kambi ya adui kwenda na kurudi wakamletea Daudi maji. Bila shaka Abishai alikuwa miongoni mwao na alifanya jambo jingine la hatari kwa upendo aliokuwa nao kwa mfalme. Lakini Daudi hakunywa maji hayo kwani yalikuwa ni sawa na kunywa damu za wale mashujaa hivyo aliyamwaga chini kama dhabihu kwa Mungu.



Kuna uhaba wa maisha ya nyakati za mwisho za Abishai lakini inaaminika alikufa kabla ya mgogoro kuhusu urithi wa kiti cha ufalme cha Daudi.
_____________________
"Kwanini huyu mbwa mfu akutukane bwana wangu Mfalme? Niruhusu nimwendee nami nitakata kichwa chake."

-Abishai.
 
Historia nzuri sana, swali je, kati ya Yoabu na Abishai nani alisimama na kuhakikisha Selemani anakuwa mfalme?
 
Historia nzuri sana, swali je, kati ya Yoabu na Abishai nani alisimama na kuhakikisha Selemani anakuwa mfalme?
yoabu aliaasi alimfuata adonia Kaka suleman wakaenda kufanya sherehe walipokuwa wakifanya sherehe mfalme daud akamtawaza Suleiman kuwa kuwa mrithi wake .Yoabu akauawa kwa sababu ya makosa yake alifanya huko nyuma aliwaua Amasa pamoja na Abneri.huyo abishai hakutajwa mwishoni historian yake haijulikan alikufaje
 

Tafuta kisa cha mfalme Nebukadneza alieongoza wayahudi wajenge mnara wa babeli kwa imani kuwa huo utakuwa uchochoro wa kuingia mbinguni.
 

Kisha tafuta kisa cha Shadraki Meshaki na Abenego waliotupwa kwenye ziwa la moto lakini hawakuungua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…