Abood Bus huduma zimeshuka na Usalama wa abiria ni mdogo sana

Abood Bus huduma zimeshuka na Usalama wa abiria ni mdogo sana

shamimuodd

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,188
Reaction score
2,113
Wadau,
Mara ya mwisho kuapa kutopanda bus za Abood ni mwezi wa pili mwanzoni, na hii ilitokana na mara kadhaa unapanda basi Dar na utakuta pale mbele kwa dereva wanajazwa watu kibao.


Na mkifika njiani wanajaza tena kama dala dala, wengine wanasimama kati kati. Na mkifika mizani basi wale abiria wanaambiwa washuke wapande dala dala au zinaandaliwa piki piki, wanakuja kupandia mbele. Wakati mwingine wale abiria wasiokuwa na siti wanaambiwa wasogee katikati.

Lingine lililonikera kabisa, yaani dereva wa hilo gari nililo panda alikuwa anaongea na mtu mwenye jina la kike (Fatuma) na inaonekana walikuwa kwenye mgogoro, dereva alikuwa anaongea na simu karibia muda wote na anajitahidi kumchimba biti Fatuma na wakati mwingine anakuwa na hasira huku gari ipo mwendo kasi sana.

Sasa ukichukulia gari imejaza watu kuzidi kiwango, spidi kubwa, nikaona hapa Abood zinakuja kuua watu wengi sana very soon.

Niliapa tangu siku hiyo Abood basi sintopanda tena labda wajirekebishe
 
Mkuu traffic police alipopanda na kuuliza "kuna tatzo" ulijibu nini?

Zile namba za Sumatra na polisi zinazobandikwa ndani hazikuwepo?

Usiogope kuwa balozi wa usalama wako. ukiulizwa kuna tatzo usiseme hakuna, sema ukweli. (Japo najua hapa wengi huofia reaction ya dereva na abilia wenzie).

MUHIMU
Pengine siyo mabasi yote ya abood hupakia kwa mtindo huo.

Naamini si dereva wote hufanya kama huyo (kuongea na simu sehemu kubwa ya safari).
Pengine hata huyo dereva naye alifanya hivyo siku hiyo tuu, kulingana na mambo yalivyokua baina yake na bi. Fatma.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
pamoja na hayo hakuna anayemzidi kihuduma kwa usafiri wa Dar Moro. hayo mayatizo bado hayana kero kama kusimama nje ya kituo cha msamvu nakusubiria abiria usiowajua, ni bonge la kero na trafki waliolikagua na kuliruhusu wakiacha tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kitu sipendi kama basi la abiria la masafa marefu kupakia watu kuzidi idadi ya seat , NAO ABIRIA ANAYEKUBALI USAFIRI WA NAMNA HIYO SIJUI VIPI? ANAKAA PALE MBELE JUU YA INJINI AU KUKALIA VINDOO ..NA UNALIPA NAULI? Kwan imekuwa enzi za ukosefu wa usafiri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom