Aboutrika aorodheshwa kwenye list ya magaidi nchi Misri

Aboutrika aorodheshwa kwenye list ya magaidi nchi Misri

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Kiungo mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Al
Ahly na Misri, Mohamed Aboutrika ameongezwa
kwenye orodha ya magaidi nchini Misri kufuatia
kutuhumiwa kuwa na uhusiano na kikundi cha
Muslim Brotherhood kilichopigwa marufuku.
Aboutrika anatuhumiwa kukifadhili kikundi cha
Brotherhood kinachotafsiriwa kama kundi la
kigaidi nchini Misri. Katika uchaguzi wa mwaka
2012, Aboutrika alimpendekeza mgombea wa
Brotherhood, Mohamed Morsi ambaye alishinda
urais na kudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja
kabla ya kung’olewa madarakani na
kuorodheshwa kwenye orodha ya magaidi nchini
humo.
Aboutrika pia amekuwa akiunga mkono nchi ya
Palestina na kuvaa fulana za kuwaunga mkono
raia wa nchi hio katika vuguvugu dhidi ya Israel.
IMG_20170118_150940.JPG

Wakili wa Aboutrika, Mohamed Osman amesema
Aboutrika ameorodheshwa kama gaidi licha ya
kutofikishwa mahakamani wala kujulishwa
kutuhumiwa.
” Tutakataa rufaa kupinga haya maamuzi,”
Amenukuliwa Osman huku Aboutrika mwenyewe
akikana tuhuma hizo.
Source: soka 360
 
Sasa gaidi halafu wanamuacha anazurula?,
 
Ukiwa muislamu unaitwa gaidi kwahiyo hadi sasa hivi kuna zaidi ya magaidi bilioni mbili na ushehe hivi hawa wote hawa mtawafanyaje ni wengi si waume si wake si watoto
 
Anaitwa gaidi kisa anapingana na uongozi uliopo madarakan uliompindua Mursi? nakuvaa fulana ya kui support palestina nao ni ugaidi??
 
Ukiwa muislamu unaitwa gaidi kwahiyo hadi sasa hivi kuna zaidi ya magaidi bilioni mbili na ushehe hivi hawa wote hawa mtawafanyaje ni wengi si waume si wake si watoto
Kwani waliomuorodhesha kwenye hiyo list siyo Waislam? Ni waislam wenziye ndiyo waliomuweka kwenye hiyo list.
 
wakati muslim broterhood wakiitwa kama magaidi na misri wenzao waturuki na qatar wao wanayaunga mkono makundi haya,

Marekani, saudi arabia,UAE, kuwait na misri wanakiita kikundi cha wanamgambo wa hputhi wa yemeni kuwa ni kikundi cha ugaidi wakati mwenzao iran anakiunga mkono......

wanamgambo wa eastern ukraine wanaopigana na serikali wanaitwa magaidi na serikali yao lakin urusi anawaunga mkono na kuwapa silaha.......

wanamgambo wanaopigana kuitoa serikali ya syria madarakan wanaitwa magaidi na urusi/syria na iran lakin marekan na wengineo wanawaunga mkono na kuwapa silaha .

wanamgambo wa hamasi wanaitwa magaidi na israel lakin nchi nyng za kiisalmu zina waunga mkono na kiwapa silaha

wakurdi wanaopigana na islamic state nchini syria uturukiinawaita magaidi lakin marekan anawasapoti na anawapa silaha za kupigana na islamic state
hebu dunia ideal na islamic state na alqeda kwanza tuyaangamize kabisa af mengne ndo yafuate maana sasa umejaa unafiki tu kila usiempenda unamuita gaidi
 
hata ANC ya mandela waliitwa magaidi
 
Mamlaka za usalama za Egypt zimemweka mchezaji wa zamani wa soka wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Mohamed Aboutrika katika ya magaidi baada ya kuhusishwa na kikundi cha waislam wa Brotherhood, amesema mwanasheria wa mchezaji huyo.
xMohamed-Aboutrika.jpg.pagespeed.ic.Rhs6iCug4l.webp

Mr Aboutrika anashutumiwa kuwasaidia kifedha kikundi cha Brotherhood, kikundi ambacho mamlaka za Misri kimewaeka kwenye kundi la magaidi.

Mnamo mwaka 2012, alimpigia kampeni ya urais Mohamed Morsi, ambaye ni mwanachama wa Brotherhood.

Jambo hilo lilipelekea kuwagawa mashabiki wa mchezaji bora wa mwaka wa BBC wa mwaka 2008.

Kwa sheria za Misri, mtu yoyote anayewekwa kwenye listi ya ugaidi, hufungiwa kusafiri na passport yake pamoja na mali zake hushikiliwa.

Mwanasheria wa Aboutrika, Mohamed Osman, alisema mteja wake hajatiwa hatiani wala hajapewa taarifa rasmi juu ya mashtaka wanayomtuhumi nayo. Pia ameahidi kukata rufaa juu ya tuhuma hizo kwa mteja wake.

Kiungo huyo wa zamani wa Al-Ahly na timu ya taifa ya Misri, alikuwa kipenzi cha wananchi wa Misri na walifikia hatua ya kumpa majina ya The Prince of Hearts, The Magician na The Saint wakati akicheza soka, lakini uamuzi wake wa kumsapoti Mohammed Morsi, ambaye alikaa madarakani kwa mwaka mmoja tu, uliwagawa mashabiki zake.

Mwaka 2015, mali zake nyingi ziliwekwa kizuiani, hisa zake kwenye makampuni tofauti zilishikiliwa na mamlaka za usalama za nchi hiyo.
 
Akamatwe na ahojiwe sio kuleta porojo za kugeukana na CIA!
 
Ukiwa muislamu unaitwa gaidi kwahiyo hadi sasa hivi kuna zaidi ya magaidi bilioni mbili na ushehe hivi hawa wote hawa mtawafanyaje ni wengi si waume si wake si watoto
Mpo bilion 1 na usheeee, usipotoshe
 
Back
Top Bottom