Hio lunch ilikuwa imewajumuisha watu kumi na sio ajabu kuona bill ikija kwa iasi hicho. Maana hapo tunazugumzia kuanzia na starters, main course na mwisho dessert. Hata hivyo main course ndio inakuwa ya nguvu na inategemea kila mtu amekula aina gani.
Kwahio hio bill ni cha mtoto kwa yeye Abramovich.
Abramovich alianza na kuuza kwenye magenge au viduka akiuza vitu vidogo vidogo na baadae akawa anauza midoli ya watoto na baadae akauza vibata vya kuweka kwenye mabafu.
Urusi ilipobadilishwa na Gorbachev ambae aliruhusu biashara binafsi, Abramovich tayari alikuwa na akiba benki kiasi cha kuingia katika biashara ya mafuta na mashamba ya mifugo ya nguruwe ambazo ndizo zimekuja kumpatia utajiri alio nao hadi leo wa karibu paundi za Uingereza billioni 11.7.
Historia ya Abramovich inapatikana katika maeneo mbalimbali zikiwemo tovuti, majarida na magazeti na unaweza kumweka katika kundi la mafisadi na hapohapo kumsifia kwa mazuri anayofanya.
Abramovich ni gavana au mbunge wa jimbo la Chukotka jimbo lililopo mashariki mwa Russia.
Yeye si kama walivyo baadhi ya wabunge wa Tanzania ambao husahau majimbo yao, ameendeleza jimbo hilo kwa kujenga mashule, makazi ya wananchi, na kuvuta wawekezaji.