Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Watanzania tusikubali kufanywa wajinga. Haingii akilini kwa viongozi wa serikali kuonyesha moyo wa upendo kwa kutembelea wahanga wa vitendo vya "kimafya" kama mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Absalom Kibanda leo huko Afrika kusini ambapo raisi amemtembelea lakini mwisho wa siku hakuna kinachofanyika licha ya ahadi za viongozi kuhakikisha wahusika wanakamatwa na kuchukuliwa hatua!
Saed kubenea alipomwagiwa tindikali viongozi wa serikali walimtembelea na kumpa pole.Dr.Ulimboka nae alitembelewa na kupewa pole.Hali kadhalika, Absalom Kibanda nae ametembelewa na kupewa pole.Na katika matukio yote haya viongozi wa serikali wana ahidi kuwa wahusika watasakwa na kuchukuliwa hatua!
Je,katika matukio yote hayo na mengine ya aina hiyo, ni watu wangapi wameshakamatwa na kufunguliwa mashitaka na hata kuhukumiwa? Sasa hii ina maana gani kama sio kuonyesha kuwa serikali haina dhamira ya kweli kushughulika wahalifu hawa?
Mimi nafikiri kama tukio hili la Kibanda litaisha kwa mtindo huu, basi ni wakati muafaka kwa wanahabari na makundi mengine ya kijamii kuweka msimamo wa pamoja kukata kutembelewa na viongozi pindi matukio hayo yanapojirudia.
Tuache kunyenyekea na kufanywa wajinga!Mbona wauaji wa aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza walipatikana!Iweji hawa wengine wasipatikane?