Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mwanahabari mkongwe Absalom Kibanda ametoa maoni yake kuhusu umuhimu wa Serikali kufanya kazi kwa ukaribu na Vyombo vya Habari ambapo kwa asilimia kubwa amelaumu mazingira ya tata baina ya pande hizo mbili.
Akitoa maoni katika Kongamano lililohusisha Wadau wa Habari, Serikali na Waandishi likiwa na kaulimbiu ya "Habari kwa Maendeleo Endelevu",jana Desemba 17, 2022 alisema:
“Mwaka 2016/17 nilipata tofauti na Rais Magufuli nilipojaribu kumshauri ni vizuri turithi kile kizuri ambacho marais wastaafu walitufundisha katika sekta ya habari.
“Kwanza Wanahabari tumewahi kutoa Rais mwanahabari ambaye ni Benjamin Mkapa, huyu alikuwa anakosoa sana Wanahabari lakini alitoa fursa sana kwa Media kupata taarifa.
“Tunaongea kuhusu fake nyuzi leo lakini hilo suala halijaanza na Mitandao ya Kijamii, ni suala la kihistoria.
“Hatujiulizi kwa nini wakati wa Mkapa au Kikwete kulikuwa na kiwango kidogo cha fake news, hata katika katika media kubwa kwa sasa inatokea fake news zinashika kasi, hiyo ni kwa kuwa waandishi wa habari hawapo sehemu nyingi za matukio.
“Mfano Rais Samia yupo Marekani ameandamana na waandishi wangapi? Nani wa Daily News ameambatana naye, vipi kuhusu TBC, Azam TV au Clouds FM, huo ndiyo mwanzo wa fake news.
“Rais alienda kuzindua Royal Tour, lakini mambo ya ajabu kabisa, Msigwa anamhoji Dkt. Abbas, huo ni uandishi gani wa habari! Tunafungua wenyewe mlango wa fake news kwa kuwa waandishi wetu hawatumiki inavyotakiwa.
“Hatujiulizi kwa nini media nyingi zinazoanzishwa leo ni za burudani na michezo, sababu upande wa serious news tumeuua.
“Leo hii vyumba vya habari Tanzania kuna generation gape, nani anawalea hao wadogo kitaaluma? Media inashindwa kwa kuwa Serikali ambaye ndiye mdau mkuu imeacha kuhusisha media ndiyo maana hazina uwezo kiuchumi.
“Kama kwenye Royal Tour, Rais aliweza kuksanya Tsh. Bilioni 7 za bajeti ya mradi huo, je mlishindwa kutenga hata Tsh. Milioni 200 kuandamana na Rais Marekani au kule Zanzibar, nadhani hapo ndipo tumekosea, naomba nitoe dokezo.”