Abubakar Mwilima

Abubakar Mwilima

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Mwaka 1951 mgogoro wa ardhi ya Wameru ulipoanza tawi la TAA mjini Tabora lilikabili changamoto hiyo kupitia juhudi binafsi za Saadan Abdu Kandoro.

Kandoro aliitisha mkutano wa matawi ya TAA ya Mwanza, Kigoma na Tabora kujadili suala hilo.

Saadan Abdu Kandoro baada ya uhuru mwaka wa 1961 aliandika kitabu, ''Wito wa Uhuru,'' (1961) kuhusu historia ya harakati hizi

Uongozi wa TAA Tabora, kwa kujihusisha katika mgogoro kama huu, ilikuja kuwa ngome ya upinzani dhidi ya ukoloni.

Joto hili lilisababisha Gavana Edward Francis Twining kutoa Government Circular No. 5 kusisitiza watumishi wa serikali kujiweka mbali na siasa.

Viongozi wa TAA walikwenda kumuona Gavana na Germano Pacha, katibu wa TAA katika Jimbo la Magharibi, alikuwa miongoni mwa wajumbe ambao tarehe walikwenda Government House kuonana na Gavana ili kujadili waraka wa serikali, yaani Government Circular No. 5 uliopiga marufuku wafanyakazi serikalini kujishughulisha na siasa.

Abubakar Mwilima wakati ule alikuwa mwalimu Tabora Town School na akatumia fursa ile kuwafungulia wazalendo wenzake darasa moja kukutana siku za Jumapili kujadili vipi waunde chama cha siasa ili kupeleka harakati mbele kutokana na Circular No. 5.

Wazalendo hawa waliokuwa wanakutana hapo Town School waliamua kumtuma Germano Pacha kwa Abdul Sykes Dar es Salaam akiwa na salamu kuwa Tabora inajitayarisha kuunda chama cha siasa.

Jibu alilopewa Pacha na Abdul Sykes ni kuwa wavute subra TAA HQ inalishughulikia jambo hilo.

Mambo yalipokuwa tayari kuwa sasa TANU inaundwa TAA Tabora ilichangisha fedha kumwezesha katibu wa TAA Jimbo la Magharibi Germano Pacha kusafiri Dar es Salaam kuhudhuria Mkutano Mkuu wa kuanzishwa TANU Julai mwaka 1954.

Mchango, mkubwa kupita yote ilikuwa shilingi ishirini.

Fedha hizi alitoa babu yangu Salum Abdallah.

Mkutano huu ulihudhuriwa na watu maarufu wa Tabora pamoja na baadhi ya waalimu kama Abubakar Mwilima, Harub Said na George Magembe.

Picha kushoto Abubakar Mwilima na Mohamed Shebe.

1655402802325.png
1655402868044.png
 
Heshima yako mzee Mohamed Said.

Msaada tafadhari maana sijaelewa vema lengo la uzi huu.

Ninaomba ufafanuzi zaidi wa bandiko lako maana wengine vichwa vinachelewa kuchakata mambo.
 
Heshima yako mzee Mohamed Said.

Msaada tafadhari maana sijaelewa vema lengo la uzi huu.

Ninaomba ufafanuzi zaidi wa bandiko lako maana wengine vichwa vinachelewa kuchakata mambo.
KII,
Lengo la uzi huu ni kusomesha historia ya TANU.
 
Assalam alleikhum sheikh Mohamed, huyu Abubakar Mwilima ana unasaba wowote na yule aliyekuwa mwandishi wa habari Suuda Mwilima? Huyu Abdu Kandoro ana unasaba wowote na huyu al marhum Said Kandoro aliyepata kuwa Mkuu wa Mkoa Dar na kisha Iringa?
 
Kile...
Bahati mbaya sijui.
 
Assalam alleikhum sheikh Mohamed, huyu Abubakar Mwilima ana unasaba wowote na yule aliyekuwa mwandishi wa habari Suuda Mwilima? Huyu Abdu Kandoro ana unasaba wowote na huyu al marhum Said Kandoro aliyepata kuwa Mkuu wa Mkoa Dar na kisha Iringa?
Sub hanallah! Kweli mitandaoni kuna kila usichokijua... Kandoro alikufa!!?
 
Sub hanallah! Kweli mitandaoni kuna kila usichokijua... Kandoro alikufa!!?
Ndio Abbas Kandoro aliyewahi kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar na kisha Iringa na baadae nafikiri aliwahi kuweka nia ya kugombea Ubunge alishafariki Dunia...kama kumbukumbu zangu ziko sawa ni miaka kama miwili au mitatu iliyopita
 
Back
Top Bottom