Abubakar Salumu 'Sure boy' apewe heshima yake

kombaME

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
2,115
Reaction score
2,818
Huyu bwana mdogo anaupiga mwingi lakini hatajwi popote, sio kwenye tuzo za soka, sio vyombo vya habari. Lakini huyu jamaa ana namba kikosi cha kwanza ndani ya timu kubwa kama Azam nadhan miaka 3 mfululizo. Ni moja ya viungo bora kabisa kutokea nchini.

Tusisubiri afe ndo tukapambe jeneza lake kwa mabendera ya club na Taifa... apewe heshima anayostahili, anaujua mpira.
 
Rekebisha hapo si miaka 3 mfululizo ni zaidi ya miaka 10 yupo Azam na namba anapata,
Sure boy is underrated
 
Abubakar Salum ni baba yake, huyu unayemzungumzia ni Salum Abubakar
 
Sure boy yuko vizuri, sema ss tumekariri tu akina Samatha, manula na wengineo
 
Nimzuri ila kipindi wa Tanzania tunaipenda timu yetu (2019afcon) alidrop nazani nimiongoni mwa wa Tz 10 waliochezea taifastarz michezo mingi
 
Watanzania wanasubiri afe ndio wammwagie masifa! Au laah wanasubiri ahamie JANGWANI ama MSIMBAZI! Yale yale ya BOCCO na NYONI!
 
Angechezea yanga na simba wangemsifu kama wenzake bocco na nyoni
 
Abubakar Salum ni baba yake, huyu unayemzungumzia ni Salum Abubakar

Kweli mkuu

Baba yake Salum Abubakari alikuwa sure boy kweli kweli, wale wasudani hawawezi kumsahau alivyotupia nao mbili dakika majeruhi kwenye nusu fainali ya klabu bingwa Africa Mashariki na kati miaka ile ya 80+
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…