Abunuasi wa Zambia

Abunuasi wa Zambia

Cesar Saint

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2016
Posts
423
Reaction score
726
Wasalaam;

Jamaa alifahamika kwa jina la Edward Makuka Nkoloso alipata kuwa Colonel wa jeshi mwalimu na mwanaharakati nchini Zambia

IMG_4798.JPG


Kubwa zaidi alikuwa National director of the science academy nchini Zambia wakati inapata uhuru mwaka 1964 na alikuwa na mpango wa kuwatupilia mbali USA na USSR(Russia) katika kipindi cha mashindano ya space exploration hasa kufika Mwezini akaenda mbali zaidi kutaka kufika kwenye sayari ya Mars kuonyesha umwamba wa Zambia katika nyanja ya sayansi na teknolojia.

IMG_4794.JPG


Kwenye mission hiyo alimuandaa binti mmoja,paka wawili na mmisionari mmoja kwaajili ya kuwahubiri injili watu wa Mars na endapo wangekataa basi wasiwalazimishe.

IMG_4793.JPG

IMG_4792.JPG

IMG_4791.JPG


Basi jamaa akafanya recruitment ya vijana kadhaa na kuwapa jina la AFRONAUTS basi bwana huyu akaanzisha mafunzo miongoni mwa routine ilikuwa kuwaweka Afronauts kwenye mapipa na kuwabingirisha kutoka vilimani na kubembea hii yote ili kuwasaidia kuwa wepesi katika kumudu safari za anga za mbali.

IMG_4795.JPG

IMG_4796.JPG

IMG_4790.JPG


D-KALU ;Yes hii ndio ilikuwa rocket/spaceship ya bwana Makuka ikitengenezwa kwa aluminum,copper na mabati akiamini ingeweza kumudu safari hizo za anga za mbali.

IMG_4786.JPG

IMG_4783.JPG

IMG_4784.JPG

IMG_4788.JPG

IMG_4787.JPG

IMG_4797.JPG



Jamaa akaomba msaada UNESCO wakati huo kiasi cha shillingi millioni 7 cha paund ya Zambia ambayo hakupata majibu akaenda kuomba donors wengine wa nchini mwake kiasi cha 1.7 billion Zambia paund ambacho pia hakuweza kupata.

Ukata wa fedha si kitu pekee kilichoikumba kambi ya Makuka tatizo kubwa lilianza pale ambapo vijana wa kiume kwenye kambi walipoanza kujihusisha na mapenzi ambapo bwana Makuka alilalamika wanapoteza umakini katika mafunzo.

IMG_4782.JPG

IMG_4789.JPG


Anguko kubwa lilitokea pale binti aliyetarajiwa kupelekwa anga za mbali aitwaye Martha Muambwa alipopata ujauzito uliowalazimu wazazi wake kumfuata na kumwondoa katika kambi ya bwana makuka.

Miaka michache baadae USA na USSR wakafanikiwa kufika mwezini na kuondoa matumaini kabisa ya bwana Makuka kutimiza ndoto zake hatimaye program hii ikafa kifo cha kimya kimya.
 
Bora hata huyo alionesha kujaribu. Hakuna yeyote ktk serikali yao aliye taka kuendeleza ndoto hiyo. Nadhan wanapambana na wale maadui watatu mpka sasa
 
He had a mission but lacking vision
Big up astronaut Makuka,
 
Write your reply...hahahaaa daaaah jameeni nipo hapa afronauts niliyemuweza space girl
 
Hongera kwa kujaribu kwake,mi nina mchezo ambao nadhani naweza kufa bila kuuanzisha kwasababu ya ukata.
Nalog off
 
Back
Top Bottom