Abuse..( Dhuluma)



MJ1 dear
asante sana
umeelezea vema na kuelimisha vizuri

Naomba kila mtu asome hapa ili tusichanganye
haya mawili jamani ni mambo mawili tofauti kabisa..

hapo kwenye red hivi kama watu wameoana na wanaishi
pamoja kwa muda lakini kila mara mmoja hajisikii kufanya sex
na mwingine akawa anamlazimishia na mara nyingine kumwingilia
kwa nguvu Je waweza sema hiyo ni abuse??

sante mpenzi kwa majibu yako ya kuaminika ...
 

asante sana kwa mtazamo wako
ningependa kukuliza ni group gani la watu
mfano.. watoto , wanawake, waume , vijana
wanaokubwa na hizo type za abuse na kwa nini
hilo group is the main target???
ntakuongezea maswali baada ya hayo ..
mmmhh Pole ae usinichukie sababu nakubana sana
hahahhahaah lol unasaidia wengi dear ..
 
Punishment ya kawaida ni kukemea,kukaripia,kofi moja wak sio mbaya ni adhabu ya kawaida,kumlaza mtoto njaa,kumfunga mikono ukamchoma moto eti kaiba sumni,kumtandika mtoto hadi vitako vikachanika,kumchezea mtoto viungo vyake .....etc hiyo ni abuse,na abuse ZOTE ni punishable by law,anayefanya abuse akidakwa ajue atakula mvua tu.
 
Haya nimerudi sasa ....
Well kuna sababu nyingi zinaweza kumfanya mtu awe mnyanyasaji.....internal na external factors hapa zote zinahusika!!

Kujiweka juu-mtu ambae yupo kwenye kundi hili ni yule anaemnyanyasa mwenzake ili yeye ajisikie kwamba ni zaidi yake.Anamchukulia
anaemnyanyasa kwamba ni DHAIFU na yeye ana nguvu.Mara nyingi watu kama hawa hua ni wadhaifu internaly kwahiyo
anatafuta wale walio wadhaifu zaidi yake ili aweze kujipa kile anachokosa ndani yake.

Lawama-Huyu ni yule ambae anatumia lawama kama kigezo cha kumnyanyasa mwingine...yani yeye haoni anakunyanyasa kwasababu
WEWE NDO UMESABABISHA.Hawa ni wale wa usiingefanya kitu flani haya yote yasiingetoea...

Visingizio-Huyu hata siku moja hawezi kusema samahani nilichofanya ni kosa ila atakwambia yote ilikua ni hasira tu....kazini wameniboa..
nilishindwa kujizuia....yani hawa wanatumia hisia zao zisizohusiana na mhusika kumnyanyasa mhusika!!

Kubadili maoni-Hawa ni wale ambae kitu kisipoenda vile alivyotarajia/taka yeye ataanza kumkashifu mwenzake kwa maneno ili ajisikie
vibaya.Mara nyingi ndo wale unaosikia wanarudishiwa kwamba wasemacho ni maneno ya mkosaji....yani kilichokua kizuri
kikiwa sio chake kinakua kibaya.Ndo unakuta watu wameachana alafu mmoja anaanza kumnyanyasa mwenzake kwa
maneno ''ahh mtu mwenyewe mbaya...sura kama mbuyu na kadha wa kadha.

Umiliki-Mnyanyasaji anasikia raha ya kummiliki mnyanyaswaji pale mnyanyaswaji anapokubali kunyanyaswa....

Hasira za haraka-Hawa ni wale ambao mikono yao na maneno yasiyo mazuri yanawatoka haraka sana.Yani hawezi kudhibiti hasira zake kiasi kwamba hafikirii anachokifanya mpaka baadae wakati ameshaharibu tayari.Hii unaweza kusema hua haitokea kwa kukusudia maana wengi wao hua wanajuta baadae.

Kisasi-Kuna watu ambao wamewahi kunyanyaswa kwahiyo ile hasira anayotembea nayo anamtolea yeyote ili kujipa yeye unafuu.Na hii inamfanya asijione mdhaifu....

Chuki-Hii wala haihitaji ufafanuzi.Mtu akikuchukia anaweza fanya chochote kukuumiza iwe kwa maneno au kwa matendo.

Kwa sababu hizo hapo juu unaweza kuona kabisa wengine wananyanyasa wenzao kwa makusudi na faida binafsi na wengine wanashindwa kujidhibiti kwasababu wana matatizo yaliyoko ndani zaidi kwahiyo sio wanyanyasaji wote ni wabaya kwa maana ya kwamba sio wote wanachagua kua walivyo.
Kuwasaidia ni ngumu sana especially wale wanaofanya kwa makusudi.Na ugumu upo kwenye kujua kama kweli mtu anpofanya vile anakua hajakusudia maana wengi hua wanaishia kulaumu kitu kingine au watu wengine zaidi ya wao binafsi. Kumsaidia inabidi ujue chanzo cha ile tabia na yeye mwenyewe atake kubadilika....siku zote huwezi kumbadili mtu kwa lazima kwahiyo inabidi mhusika mwenyewe aseme kweli sipendi kua hivi na nasikia uchungu kwa ninayo/niliyofanya.
Ikiwa anataka kubadilika kwanza inabidi ajitambue yeye kama mnyanyasaji ....ajichunguze ndani yake kujua sababu na awe anajutia matendo/maneno yake.Ikifuatiwa na kumfanya ajisikie vile anavyofanya wenzake wajisikie...hii itamfanya ahisi huruma....alafu kutokana na majuto yake ajue kwamba anapofanya vile haimsaidii hata yeye maana at the end of the day anaishiia kulilia msamaha.Baada ya hapo aface hicho kinachomfanya awe vile ili aweze kuondokana nacho.
 


eeee
kweli umeongea cha maana sana kuhusu US dahhh
mimi topic yangu ilikuwa ina target familia na jamii tuu
kumbe hata nchi na nchi zina dhulumiana dahhhh
asante kwa kunifungua macho dear ..

nway Je mafano baba ni mnywaji sana
baba anampiga mama kila jua likizama,
anatukana hajali nani ni nani anachukia
familia yake for no reason anatekeleza familia every now and then
Je kama kuna mtoto wa kiume aliye kulia kwenye familia ya namna
hiyo , unadhani atakuwa kama baba yake kwa kiasi fulani akikua??
au unadhani baba kuwa hivyo ita muaffect vipi(mtoto) katika maisha yake??
 


In red.. Asante kwa kunielewesha hilo...Hivyo Noted.

In nyeusi bolded... Bahati nzuri au mbaya huwa katika jamvi ni vigumu kumfahamu mtu vizuri because hua tunaanika yale ambayo tuko comfortable to admit... Nikisema hua sikubali kitu kama hicho (hasa mambo yamhusuyo mwanamama underpreviledged na children) kikifanyika na am aware nikae kimya - hope you believe...Nasema hivi sababu katika hili suala la sexual abuse na molestation ni suala ambalo liko saana katika jamii but kwa kujificha mno, maeneo ninayoishi yaweza changia nisishudie mara kwa mara but ukweli unabaki kua ni wengi.... Kitu kama hicho kimetokea na najua si rumors ni kweli kabisa hata kama hio family siwafahamu nitaingilia kati mana siwezi condone...Kuingilia kunategemea mambo mengi tokana na jamii yetu jinsi ilivyo, wahusika ni wanafamilia ama si wanafamilia, victim ana ndugu ama hana ndugu au mtu wa kum-support, victim anataka iwe reported ama lah! Umri wa huyo victim ni under 14, under 18 au over that age... Hivyo vitu ndio vita determine ni namna gani naweza msaidia - kwamba imekaa kifamilia au ki chombo husika....

Kuhusu kukwazika AD mtu ukija katika jamvi hili la GT ukifikiri unajua kila kitu na what you know ndo ukweli naamini kwa mtazamo wangu kua such a person has to be disqulified... Tunakutana na kupeana mawazo mbali mbali, tunaongeza maarifa, knowledge, tunagusia mambo ya jamii na most importantly kusikia maoni ya wengi ambao mtu lazima utatoka na moja kama si mawili.... Hivyo AD mimi napenda sana mtu kunirekebisha nilipokosea for that is how we become mo' knowledgeable and wise... Like i said before nimependa observation yako...
 
AD yote tisa,mi ugomvi wangu ni hapo kwenye red,yaani kila kukicha dhulma zote ni sisi kina baba tunawatendea mama zenu,ya kweli hayo? Mangapi ya ajabu na kusikitisha kina mama wanawatenda waume zao wengine hadi kuwasababishia vifo tena wakati mwingine wakishirikiana na mabinti zao?
 



nnunu... nini naweza ongea hapa....I AM ALWAYS IN AGREEMENT WITH YOU... Asante kwa ile fidbak.
 

Unajua AD maisha ya ndoa are very complicated si straight forward kama wengi wetu tunavyofikiria.............. kwa kuanzia tu ni vema kujua nini kinasababisha kwa mtendwa kutokuwa na hamu ya kusex na mume/mke wake kabla ya kumuhukumu mume/mke aliyeforce sex. Kuna mengi hapo huchangia and we have to be makini kutohukumu pasipo kuanalyse yalotokea au sababisha

Definetly it is not acceptable kuforce sex from your spouse ...not at all BUT...kama kweli unampenda and you deny him/her of sexual pleasure unategemea akapate wapi?.......to some extent.......kama hujui chanzo its better not to jump into conclusion......sometimes it is better to be bakwad (kistaarabu lakini) by your hubby/wifey than letting him go and quench his thirst somewhere else....kama huna sababu ya msingi ya kudeny him of his righ.(Mkinishambulia mnishambulie tu)
 

my dear asante sana
simpe and well explained..

samahani kwa swali hili..
Je we unadhani kwa familia za hapa
kwetu Tanzania ni rahisi kwa mtu ku
report kitu kama hicho ???
 
hahahaha...nimependa topic yako sana. Lazima nikubali hapa kuwa mimi natumia verbal abuse sana, lakini sio kwa marafiki au ndugu bali kwa wafanyakazi wenzangu. Sijajua tatizo...nitachunguza zaidi kesho nikienda kazini...
 
daahhh
Hivi hii topic ni ngumu kiasi hicho???
naona kila mtu anakimbia mmmhh

Hii topic ina mambo mengi sana my dia
Yaani ni kama umekusanya mafaili ya ofisi tatu za Mamlaka za Kodi nchi za USA, China na Brazil halafu umeweka ktk kajidude kamoja kadogo (flash)

Kwanza naomba nikurekebishe kwamba Sexual Abuse tunatafsiri kwa kiswahili kama Unyanyasaji wa Kijinsia



Naomba sasa nielezee kisa kimoja cha Unyanyasaji wa Kijinsia.

Kuna mdada ana mtoto mmja ameolewa, ana miaka minne katika ndoa yake, alizaliwa miaka 24 iliyopita.
Yeye na mume wake walikua wana pendana sana na mpaka sasa mdada anasema bado anampenda tena sana mume wake.

Ananiambia, " Yaani CPU, siku hizi mume wangu kabadilika sana kiasi najuta hata kuolewa yaani kidogo kanitukana mara mshenzi mara mjinga mara ananitisha kunipiga kwa kusema mimi simjui vizuri ndio maana nashindwa kufanya atakavyo.

Ukweli ninachanganyikiwa mume wangu anakuwa kigeugeu anaweza akakwambia "mimi sipendi uvae nguo ndefu", ukivaa fupi kwa muda huo aliosema anafurahi sasa itokee siku nyingine akuambie tutoke ukivaa hiyo nguo fupi anaanza
" . . . . unaenda kumuonyesha nani? Unatakautongozwe kwani mimi sikutoshi? "
Ukivaa ndefu au suruali ananyamaza.

Juzi simu yangu ilijizima nikiwa salon iliyo nje ya uzio wa nyumba tunayo ishi. Akampigia rafiki yake akaja mpaka saloon nikaongea naye kupitia simu ya rafiki yake. Jamani hakutaka kukata simu mpaka muda wa kazi uishe, karudi home hakuna salam ananiambia "utanieleza uliko kuwa" huku anatafuta mkanda aanze shunghuli. Mimi nikamwambia mimi sijatoka hata gengeni sikwenda.

Siku hiyo ndipo alipo mwita mtoto wake mwenye miaka minne nilimkuta naye akamuuliza, ndipo mtoto akamwambia "mama leo hajaenda mahali zaidi ya saloon anako sema" mume wangu akaona aibu akaondoka.

CPU, hata sasa nikimuuliza kwa nini ananifanyia hivyo ananiambia nisimkumbushe anakasirika mpaka nashindwa hata kuendelea kumuuliza. Ni mengi lakini naomba unisaidie "
 
Tabia ni kama ngozi ya mwili na mtoto wa nyoka ni nyoka;
Hivi vitu vilikuweko toka enzi za babu yetu DAUDI kwani alimdhulumu askari wake mke tena akampeleka vitani ili auawe ndo aweze kumla mjane kwa raha zake.

Haya mambo ni takribani 95% ya mambo yatendekayo duniani, halafu 5% ni usamaria wema ambao usipokaa vizuri unapigwa changa la macho pia.
 
my dear asante sana
simpe and well explained..

samahani kwa swali hili..
Je we unadhani kwa familia za hapa
kwetu Tanzania ni rahisi kwa mtu ku
report kitu kama hicho ???
Oh dear siku hizi mbona watu wengi wamefungwa sana tu.Zamani jinai hizi zilikuwa haziadhibiwi kwa sababu ya ukimya wa jamii,siku hizi watu wameamka,wakiona mathalan mtoto kafanyiwa mbaya wanachofanya ni kumtonya mwandishi wa habari(wamejaa tele mitaani tunakoishi),akishaaandika tu kwenye gazeti/TV/radio -hasa kipindi cha clouds 'Leo tena' saa 3 asubuhi,Kova akisikia tu wangu wangu anatuma vijana wa kazi maana anajua kesho yake media itamdai mrejesho.
 


dahhh
asante sana kweli
umeelezea kwa kina na kirefu sana asante
nilichogundua hapa unasema kwamba hao watu wanao abuse wengine
wanafanya hivyo ili kujitosheleza walichokosa au kufurahisha nafsi zao..

Je unadhani mtu wa namna hiyo
ataweza kuacha hayo mambo peke yake
au anahitaji some series Help??
 

Pole kwa kutendwa
 

I am super impressed with your answer
very smart thank you so much..
one more thing hapo kwenye red
Hivi kweli inajalisha kama anataka au la??
kama mtu yuko kwenye abuse relation na
anampenda sana mumewe na akisema
hataki u report na we unajua sana hali si nzuri
hivi kweli itajalisha hapo??
 

my dear samhani sana
ila huo ni mfano tu ..
na nimeweka hivyo maana
ni majority (wanawake na watoto)
mara nyingi lakini kweli kuna
wanawake wengine ni sumu pia..
samahani kama nimekukwaza
 

hahahahaahahaha lol
MJ1 bwana hapo kwenye red
umenichekesha kwa kweli lahhh

Nway leo tunaongela kuhusu hizo dhuluma tu..
mambo ya ndoa sintoingilia sana leo..ila nashukuru sana
na asante sana kwa majibu yako ya kistaarabu na ya kueleweka..

naacha kukuchimba maswali sasa hahahahhaah lol
lakini ukipata cha kuongezea au kusema
your more than welcome...
sante sana dada mzuri
God bless
 
hahahaha...nimependa topic yako sana. Lazima nikubali hapa kuwa mimi natumia verbal abuse sana, lakini sio kwa marafiki au ndugu bali kwa wafanyakazi wenzangu. Sijajua tatizo...nitachunguza zaidi kesho nikienda kazini...

mmmmhhhhhh
we ni fujo nyingi tu
mi si nakujua wewe
hahahaaahh lol

Hivi wana respond vipi kwako
pale unaporopoka kama uji wa ugali
hahahahha lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…