Abuu, Ishaka Marande na Yakub "Gowon" Mbamba

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
ABUU, ISHAKA MARANDE NA YAKUB "GOWON" MBAMBA

Mazishi hapa Dar es Salaam yamekuwa mahali pa kuwakutanisha watu ambao hawajaonana miaka mingi sana.

Ilikuwa leo mchana Masjid Nur Magomeni tumekusanyika tunasalia jeneza la ndugu yetu Rubea.

Ukoo wa Rubea ni maarufu Bagamoyo, Zanzibar na Dar-es-Salaam.

Msikiti umejaa pomoni.

Wakati tunapanga safu kuna mtu kanishika bega kwa nyuma.
Nageuka.

Waingereza wanasema, "Split second," yaani muda mdogo chini ya sekunde.

Kwa muda mdogo sana sikuweza kumtambua.
Hapo hapo lakini nikaita jina, "Marande!"

Tabu kuamini yapata miaka 40 imepita mimi na Ishaka Marande hatujaonana ingawa humuuliza kwa watu Marande yuko wapi?

Tunajaza safu tusali.

Nimemuona Abuu kwa nyuma safu ya mbele yangu na nimemtambua mara moja.

Abuu tunakutana sana na mara nyingi; na tukikutana tunazungumza kefu yetu.

Uhusiano wetu ulijengeka zaidi katika miaka ya mwanzoni pale wanetu wa kiume walipokuwa wanasoma shule moja Kenya.

Mwanangu aliporudi likizo akaniambia, "Baba nasoma na mtoto wa Abuu anasema wewe lazima baba yake utamjua kwani alikuwa mchezaji mpira maarufu wa Cosmopolitan."

Jibu langu kwake lilikuwa, "Maarufu."

Turejee kwa Marande.

Tulipomaliza shughuli ndani ya msikiti neno nililomwambia ilikuwa, "Marande ukicheza mpira..."

Marande alitabasamu.
Marande kwangu mimi ni kaka mkubwa.

Katika miaka ya 1950 Marande na dada yake mdogo Mgeni wakisoma chuo cha Shariff Abdulrahman na dada yangu mkubwa.

Chuo hiki kilikuwa Mtaa wa Sukuma na Mafia mkabala na club ya Yanga.

Nikamuuliza Marande dada yake Bi. Mgeni yuko wapi kwani nina miaka sijamtia machoni.

Picha hiyo hapo chini Ishaka Marande ni huyo kulia, anafuatia Abuu na wa mwisho ni Yakubu Mbamba.

Mwaka wa 1966 General Yacub Gowon alipochukua uongozi wa serikali Nigeria kwa mapinduzi tukambadili jina Yakubu wetu tukampachika jina la Gowon.

Akawa Yakubu Gowon.
Jina hili limemganda hadi leo.

Yakubu alikuwa na mpira mzuri sana Mashaallah alicheza Saigon, Dundee na Congo United (Shetani Wekundu).

Na mimi nazijua sifa zake nyingine mbili ninazozipenda kwake.

Kwanza upole na pili Yakubu ni "Dandy" anajua kuvaa.

Mwangalie kwenye hiyo picha kavaa "blazer" nyeupe ndani T Shirt nyeupe na kichwani katundika tarbush.

Tulipokuwa wadogo tuko shule ya msingi tukiimba nyimbo moja, "Kofia nyekundu tarbushi yakupendeza...hao Wanyiramba..."

Abuu alikuwa beki kigingi Cosmo.
"Hard tackler."

Kuna kisa mechi ya Yanga na Cosmo Ilala Stadium Abuu alipambana na Kitwana Manara.

In Shaa Allah iko siku nitakihadithia.

Marande akicheza "mid field."
Hata sijui niseme nini.

Stamina, ball control, stylish...
Akipendeza kwenye jezi.

Wakati ule Cosmo ikitisha.
Tommy Sithole mwandishi wa michezo akiwaita, "Giant Killers."

Timu ilisheheni nyota watupu: Ishaka Marande, Kesi Kibuda, Kitwana Douglas, Iddi Balozi, Jamil "Denis Law" Hizam, Said Ndomo, Hamis (Marlon Brando), Msuba, Mohamed Msomali, Mohamed Aden, Emil Kondo (Mzungu), Said Nassor, Mohamed Msomali, Mohamed Aden, Haroub (N'nge), Makanda "Norman Hines" Tambaza, Abdimout, Masiku (Mkoloni) golini na Coach Mansur Magram.

Dar es Salaam ile ilikuwa na raha zake.

1713726247573.png

Kulia: Ishaka Marande, Abuu na Yakub Mbamba​
 
Hongera Mzee Mohamed,mbona hakuna jina la kikristo katika hao wachezaji🤣
 
ABUU, ISHAKA MARANDE NA YAKUB "GOWON" MBAMBA

Mazishi hapa Dar es Salaam yamekuwa mahali pa kuwakutanisha watu ambao hawajaonana miaka mingi sana.

Ilikuwa leo mchana Masjid Nur Magomeni tumekusanyika tunasalia jeneza la ndugu yetu Rubea.

Ukoo wa Rubea ni maarufu Bagamoyo, Zanzibar na Dar-es-Salaam.

Msikiti umejaa pomoni.

Wakati tunapanga safu kuna mtu kanishika bega kwa nyuma.
Nageuka.

Waingereza wanasema, "Split second," yaani muda mdogo chini ya sekunde.

Kwa muda mdogo sana sikuweza kumtambua.
Hapo hapo lakini nikaita jina, "Marande!"

Tabu kuamini yapata miaka 40 imepita mimi na Ishaka Marande hatujaonana ingawa humuuliza kwa watu Marande yuko wapi?

Tunajaza safu tusali.

Nimemuona Abuu kwa nyuma safu ya mbele yangu na nimemtambua mara moja.

Abuu tunakutana sana na mara nyingi; na tukikutana tunazungumza kefu yetu.

Uhusiano wetu ulijengeka zaidi katika miaka ya mwanzoni pale wanetu wa kiume walipokuwa wanasoma shule moja Kenya.

Mwanangu aliporudi likizo akaniambia, "Baba nasoma na mtoto wa Abuu anasema wewe lazima baba yake utamjua kwani alikuwa mchezaji mpira maarufu wa Cosmopolitan."

Jibu langu kwake lilikuwa, "Maarufu."

Turejee kwa Marande.

Tulipomaliza shughuli ndani ya msikiti neno nililomwambia ilikuwa, "Marande ukicheza mpira..."

Marande alitabasamu.
Marande kwangu mimi ni kaka mkubwa.

Katika miaka ya 1950 Marande na dada yake mdogo Mgeni wakisoma chuo cha Shariff Abdulrahman na dada yangu mkubwa.

Chuo hiki kilikuwa Mtaa wa Sukuma na Mafia mkabala na club ya Yanga.

Nikamuuliza Marande dada yake Bi. Mgeni yuko wapi kwani nina miaka sijamtia machoni.

Picha hiyo hapo chini Ishaka Marande ni huyo kulia, anafuatia Abuu na wa mwisho ni Yakubu Mbamba.

Mwaka wa 1966 General Yacub Gowon alipochukua uongozi wa serikali Nigeria kwa mapinduzi tukambadili jina Yakubu wetu tukampachika jina la Gowon.

Akawa Yakubu Gowon.
Jina hili limemganda hadi leo.

Yakubu alikuwa na mpira mzuri sana Mashaallah alicheza Saigon, Dundee na Congo United (Shetani Wekundu).

Na mimi nazijua sifa zake nyingine mbili ninazozipenda kwake.

Kwanza upole na pili Yakubu ni "Dandy" anajua kuvaa.

Mwangalie kwenye hiyo picha kavaa "blazer" nyeupe ndani T Shirt nyeupe na kichwani katundika tarbush.

Tulipokuwa wadogo tuko shule ya msingi tukiimba nyimbo moja, "Kofia nyekundu tarbushi yakupendeza...hao Wanyiramba..."

Abuu alikuwa beki kigingi Cosmo.
"Hard tackler."

Kuna kisa mechi ya Yanga na Cosmo Ilala Stadium Abuu alipambana na Kitwana Manara.

In Shaa Allah iko siku nitakihadithia.

Marande akicheza "mid field."
Hata sijui niseme nini.

Stamina, ball control, stylish...
Akipendeza kwenye jezi.

Wakati ule Cosmo ikitisha.
Tommy Sithole mwandishi wa michezo akiwaita, "Giant Killers."

Timu ilisheheni nyota watupu: Ishaka Marande, Kesi Kibuda, Kitwana Douglas, Iddi Balozi, Jamil "Denis Law" Hizam, Said Ndomo, Hamis (Marlon Brando), Msuba, Said Nassor, Haroub (N' nge), Makanda "Norman Hines" Tambaza, Masiku (Mkoloni) golini na Coach Mansur Magram.

Dar es Salaam ile ilikuwa na raha zake.

View attachment 2970467
Kulia: Ishaka Marande, Abuu na Yakub Mbamba​
 
Sh Mohamed
Leo ninakuvulia kofia kwa kunikumbusha Dundee, kweli wasemavyo “wakati ni upepo”
Jee nikuulize mtaa wa Ungoni unapajua? Najua sana kuwa unapajua lakini tuyawache kama yalivyo, sisi ni wadogo kwenu,
Kweli usemayo watu hawaonani mpaka kwenye maziko, Mwenyeezi Mungu awasamehe wote waliotangulia
Mwenyeezi Mungu akujaaliye kila lenye kheri na wewe na akuepushe na shari
 
Mzee saidi umesahau kuelezea jinsi alivomsaidia Nyerere na pia hujaweka wazi alitoa nyumba ipi iwe ofisi ya TANU
 
Sh Mohamed
Leo ninakuvulia kofia kwa kunikumbusha Dundee, kweli wasemavyo “wakati ni upepo”
Jee nikuulize mtaa wa Ungoni unapajua? Najua sana kuwa unapajua lakini tuyawache kama yalivyo, sisi ni wadogo kwenu,
Kweli usemayo watu hawaonani mpaka kwenye maziko, Mwenyeezi Mungu awasamehe wote waliotangulia
Mwenyeezi Mungu akujaaliye kila lenye kheri na wewe na akuepushe na shari
Wandugu...
Amin.

Dundee United.
Umenikumbusha rafiki na mzungumzaji wangu Sadiki ''Kitonsa,'' Ngwira, Omar Issa, Hamisi Tumbo na wengine wengi.
 
Mzee Said humu kuna wajukuu zako pengine mpaka vijukuu hivyo wengine hufanya kama utani wa babu wa wajukuu ,basi karibu Sakura Pangani Tanga

Njumu...
Hapa waliopo ni umri wa watoto wangu.
Wajukuu zangu hata sekondari bado hawajafika.

Kitu kimoja ningependa sana kifahamike.

Katika haya ambayo mimi naandika hapa JF si mambo ya maskhara ya watu kufanya utani.

Nilifika Sakura na Kipumbwi 2003 na Dr. Harith Ghassany wakati akitafiti historia ya mapinduzi ya Zanzibar kuangalia ilipokuwa kambi ya Wamakonde waliovushwa kuingia Zanzibar kupigia kura ASP na kusaidia katika kuiangusha serikali ya Sheikh Mohamed Shamte.

Tuliletwa huko na Mohamed Omari Mkwawa.
Dr. Ghassany akaandika kitabu maarufu: Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru (2010).

Tulifika hadi Pangani mjini.
Ahsante kwa kunialika mjini kwako.

1713879214714.jpeg

Kipumbwi 2003
1713879533656.png

Mohamed Omari Mkwawa​
 
Back
Top Bottom