AC ya gari haitoi baridi kabisa

AC ya gari haitoi baridi kabisa

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Habari.
AC katika gari yangu haitoi ubaridi kabisa. Inatoa upepo kwa nguvu tu, ila upepo hauna ubaridi wowote.

Mfano, jana nilijaribu kuwasha feni hadi mwisho nikiwa nimezima AC na nikiwa nimewasha AC. Hakuna utofauti kabisa.

Kama haitoshi, nikiwa nimewasha feni hadi mwisho, nikaongeza joto hadi mwisho (32 Degrees of Celsius) lakini sikuona utofauti wowote na nikiweka baridi hadi mwisho (16 Degrees of Celsius).

Kwa kifupi, feni inatoa upepo vizuri tu, lakini ubaridi hakuna kabisa.

Gari langu ni jeusi kwahiyo na joto ili la Dar (mfano jana niliona 36 Degrees) jumlisha na foreni, raha ya gari siioni sana.

Msaada wa mawazo, fundi au ushauri wowote.

Location: Ubungo, kama aina ya gari ina matter ni Runx 2002.
 
Kuna Mawili.
1. Gas ya AC imeisha, ( ingawa ni nadra sana)
2. Kuna Chujio la kuchuja Vumbi, kama sponchi, ikiwa imejaa Vumbi huwa inasababisha hio hali na pia gar inakuwa haina nguvu ukiwasha AC na ukiwa unapandisha Mlima. chujio huwa linabadilishwa, na kulingana na gari bei huanzia 5K - 30K
 
Nitajaribu kucheki hayo mawili.
Kuna Mawili.
1. Gas ya AC imeisha, ( ingawa ni nadra sana)
2. Kuna Chujio la kuchuja Vumbi, kama sponchi, ikiwa imejaa Vumbi huwa inasababisha hio hali na pia gar inakuwa haina nguvu ukiwasha AC na ukiwa unapandisha Mlima. chujio huwa linabadilishwa, na kulingana na gari bei huanzia 5K - 30K
 
Compressor pia inaweza kuwa na shida. Unaweza kutest kwa kuangalia kama inaengage kwenye pulley inayozungushwa na mkanda wa engine. Fungua bonnet, washa gari wakati AC imezimwa, utaona pulley ya compressor haizunguki. Then washa AC, kama bado haizunguki, inaweza kuwa ni hiyo.
 
Na mimi nina tatizo hilo hilo...ila kwangu compressor ina ingage vizuri tatizo ni hakuna ubaridi na nikiweka joto..napata joto la kutosha tu...tatizo laweza kuwa nini
 
Jaribu kuangalia haya mambo mawili utapata jibu sahihi juu ya hiyo shida..

La kwanza washa gari yako harafu funua bonet washa ac angalia kama ile clutch ya compresorr ime engage na inazunguka..kama NO haizunguki basi shida inaanzia hapo..

Kama haizunguki basi kuna mambo mawili yanayoweza kusababisha
La kwanza shida upande wa umeme?? Umeme haufanyi kazi au haufiki kubana compressor??..

La pili gari haina gesi..gari ikiwa haina gesi compressor haiwezi kubana..

Kutambua kama gari ina gesi ni rahisi kwenye pipe ya ac huwa kuna kuwa na kifuniko fungua chukua kijiti bonyeza uone kama kuna gesi hapo kuwa makini na macho usielekeza macho hapo hapo unapo bonyeza..pili yatakiwa gesi itoke na sio hewa ya pressure..

Na kama gari ina shida ya gesi imekwisha nenda kwa fundi sio akujazie gesi bali akafuatilie sehem yenye likage na sio kujaza tuu gesi..maana gesi huwaga haiishi ikiisha basi kuna mahali inavuja
 
Habari.
AC katika gari yangu haitoi ubaridi kabisa. Inatoa upepo kwa nguvu tu, ila upepo hauna ubaridi wowote.

Mfano, jana nilijaribu kuwasha feni hadi mwisho nikiwa nimezima AC na nikiwa nimewasha AC. Hakuna utofauti kabisa.

Kama haitoshi, nikiwa nimewasha feni hadi mwisho, nikaongeza joto hadi mwisho (32 Degrees of Celsius) lakini sikuona utofauti wowote na nikiweka baridi hadi mwisho (16 Degrees of Celsius).

Kwa kifupi, feni inatoa upepo vizuri tu, lakini ubaridi hakuna kabisa.

Gari langu ni jeusi kwahiyo na joto ili la Dar (mfano jana niliona 36 Degrees) jumlisha na foreni, raha ya gari siioni sana.

Msaada wa mawazo, fundi au ushauri wowote.

Location: Ubungo, kama aina ya gari ina matter ni Runx 2002.

Umeishiwa Freon (gesi ya ubaridi), kajaze.
 
Cha muhimu wakat wa kujaza gas angalia kama kuna likage kama alivyosema mdau hapo juu...toyota ni mojawapo ya gari zenye ac nzuri sn
 
Back
Top Bottom