Acha kuiga tabia za watu waliofanikiwa

Thamani Academy

New Member
Joined
Jul 25, 2020
Posts
4
Reaction score
3
Ninatambua sana kwamba, wamekufundisha na kukuambia "Utafute Role Model" na uige kile anachokifanya ili uweze kufanikiwa kama yeye. Wamekufundisha pia kusoma vitabu vya Mafanikio na kufuata kile kilichoandikwa humo.⁣

Mimi leo ninataka kukuambia ukweli. Ukweli utakaobadili maisha yako. Upo tayari kusikia ukweli huu?⁣

"𝘜𝘯𝘢𝘶𝘢 𝘶𝘸𝘦𝘻𝘰 𝘸𝘢𝘬𝘰, 𝘶𝘯𝘢𝘶𝘢 𝘶𝘣𝘶𝘯𝘪𝘧𝘶 𝘸𝘢𝘬𝘰 𝘯𝘢 𝘶𝘯𝘢𝘶𝘢 𝘬𝘪𝘱𝘢𝘫𝘪 𝘤𝘩𝘢𝘬𝘰 𝘬𝘸𝘢 𝘬𝘶𝘪𝘨𝘢 𝘫𝘪𝘯𝘴𝘪 𝘢𝘯𝘢𝘷𝘺𝘰𝘧𝘢𝘯𝘺𝘢/𝘢𝘭𝘪𝘷𝘺𝘰𝘧𝘢𝘯𝘺𝘢 𝘮𝘵𝘶 𝘮𝘸𝘪𝘯𝘨𝘪𝘯𝘦"⁣

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kujifunza namna ya kufanikiwa na kujenga Biashara au mfumo utakaokusaidia kufikia mafanikio halisi

Hii ni sawa na utofauti uliopo katika ya "Kipaji" na "Juhudi". Kuna watu wengi sana wenye vipaji, lakini hawana mchango wowote hapa duniani (Kwa sababu ya kutotumia vipaji vyao). Na kuna watu hawana kabisa vipaji vikubwa, lakini wanamchango mkubwa sana hapa duniani (Kutokana na Juhudi zao).

Ni sahihi kabisa kupata Maarifa na Kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa. Lakini SI SAHIHI "Kuiga" kile walichokifanya/wanachokifanya.

Kuna msemo wa Kiingereza unasema "The Struggle is REAL" Maana yake, zile changamoto utakazozipitia kwa kujenga kitu chako, kwa kutumia ubunifu wako, juhudi na Maarifa, ndio chachu ya Mafanikio yako

Kwa maana hiyo, ni muhimu sana upitie changamoto Halisi kwa kujenga mfumo utakaokufaa wewe mwenyewe, kitu ambacho watu wengi hukimbia na kuishia kuiga vile wanavyofanya watu wengine.

Mafanikio hayana Fomula inayofanana kwa kila mtu. Kujifunza njia aliyopita mtu mwingine haina maana na wewe ni lazima upite njia hiyo hiyo. Katika mafanikio, wewe una sehemu yako, na ni wewe tu ndio utakaepita njia hiyo na wala si mtu mwingine.⁣

Hebu niambie, Ulishawahi kuiga Jinsi anavyofanya mtu mwingine? Matokeo yalikuwaje?⁣

Let's Meet again[emoji1666]

#weweniwathamani (Mtu mwingine Asikuambie Tofauti).
 
Ndo yale Yale,
Umetoka familia maskini,huna elim,huna pesa Wala huna biashara yoyote hata ya kumuingizia elfu 5 kwa siku.

Afu unakuja kusema roll model wako Ni MO DEWJI.

Atapambana kufa na kupona awe Kama MO

Huwa namuuliza,
Hivi Utajifunza Nini kwa mtu Kama MO ambae alizaliwa akaikuta pesa iko kwenye njia yake.

Mtu ambae alisomeshwa elimu maksudi kabisa akiandaliwa kuja kurithi biashara.

Mtu ambae, hajawah kuhesabu kenchi usiku au kula ugali na uji Kama yeye.

Nkamshauri Ni Bora atafute roll model mwenye background ambayo inaendana angalau na alikotokea.

Amhamasishe katika upambanaji.

Vinginevyo, ITAKUA NI SAWA NA KUJILISHA UPEPO.
 
Darasa aliwahi kusema ukiniuliza nataka kuwa nani nakwambia nataka kuwa MIMI, lakini sio mbaya ukapa mifano hai na uzoefu kwa waliofanikiwa sababu naamini pia kabla ya kufanikiwa walianguaka sana kisha kuinuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…