Acha kusikilizia mchongo, amka ukapambane

Acha kusikilizia mchongo, amka ukapambane

o_2

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2017
Posts
428
Reaction score
385
Nayee?

Miaka mingi iliyopita, miaka ya tisini kuja elfu mbili. Kuna watu wanajiuliza tisini juzi tu!? Leo ni miaka 30 iliyopita, vijana waliobahatika kwenda shule walipata ajira serikalini kwenye taasisi mbalimbali. Waliobaki wakiendelea na kilimo, ufugaji na shughuli zingine za kujiongezea kipato biashara.

Miaka ya elfu mbili waliojitafuta wakajipata, ndio wakaanza kuonekana na 'vitu vitu' mafanikio ya jasho zao yakaanza kuonekana.

Wale wa kesho itajihangaikia yenyewe, gepu likaanza kuonekana, utegemezi....kwa wale walioanza kufanikiwa. Hapo nazungumzia waliozaliwa miaka ya sabini na themanini.

Waliozaliwa miaka ya tisini mambo ni yale yale waliofanikiwa, utegemezi kwa wale waliozaliwa miaka ya themanini, yaleyale. Wa miaka ya elfu mbili waliojipata wametengeneza circle yao.

Hapa nazungumzia wale wenzangu na mimi ambao tupo tunaandika hadithi zetu.

Vijana wengi sana tupo kwenye shimo la kusoma kuajiriwa. Na hili tutaendelea kulaumiana siku zote nimesoma lakini kazi hakuna. Kutengeneza chuki dhidi ya walionacho na wenye mamlaka haiwezi kuwa suluhisho.

Suluhisho ni kubadilika na kuamua kujipambanua, kufanya kazi halali. Hatuwezi kukaaa muda wote kijiweni kupiga story za boli na mambo ya siasa wakati familia zetu zilishatrngeneza utegemezi kwa sisi ambao bado hatujajipata.

AMKA sasa, toka magetoni, fursa zipo nyingi..jichanganye upate doo kesho mwanao asije kuwa tegemezi. Wapo waliomaliza vyuo tokea 2015 mpaka leo wanasikilizia ajira za gavoo. Privates zipo kibao, hamtaki. 'Nasikilizia MCHONGO' haijawahi kuwa suluhisho.

Weka vyeti mkali. Nenda shamba, nenda kariakoo, fanya chochote halali ilimradi utengeneze kipato ili kesho tukikaa tunawaangalia wa miaka ya elfu mbili na mambo yao.

AMKA mwanangu.
 
😁😁😁 twafiq
The ability and opportunity to succeed maamaee
il_794xN.2160374853_o00v.jpg
 
Back
Top Bottom