Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
ACHA KUZUGA; MAISHA HAYANAGA KISINGIZIO.
Anaandika, Robert Heriel.
Yule Mtibeli.
Maisha hayakuzugi, hayachezi na wewe, hayana mzaha, yapo halisi, ni tukio Linaloenda mubashara ambalo hakuna kuhaririwa, maisha hayanaga kisingizio, hayabahatishi na hayapo kibahati bahati, ingawaje wahusika ambao ni Sisi tunaweza kuwa tulikuja Kwa nasibu tuu, Kwa bahati.
Ili ufanikiwe katika Jambo lolote katika maisha, yapaswa uwe sehemu ya maisha yenyewe, ufanane nayo, uyaishi na sio uishie, usiwe mtu wa Kuzuga kwani maisha hayazugi, usihitaji muda wa kueditiwa(second chance), Bali uwe mubashara, kwani maisha hayatoi second chance, usiwe mtu wa visingizio kwani maisha hayanaga visingizio, usiwe mtu wa kubahatisha kwani maisha sio ya kubahatisha, maisha yapo yanahitaji watu waliopo na sio Wale wanafikiri leo wapo kesho hawapo.
Acha Kuzuga, maisha yatakuzingua, Acha visingizio usije ukapigwa KO na Maisha.
Watu wanaozuga kwenye maisha ni Wale wanaoishi Bora kuishi, wao hufikiri kuwa maisha ni bahati na wengi wenye Mtazamo huu wameonja joto la jiwe, maisha ni uhakika watu wa dini huita IMANI, Yaani sio kubahatisha. Na watu wenye uhakika hawabahatishi kwani wamekuwa sehemu ya hayo maisha. Maisha ndio wao na wao ndio hayohayo maisha.
Maisha yanahitaji nguvu, akili, na moyo wote ili ufanikiwe.
Jambo lolote usipolifanya Kwa nguvu zako zote, Kwa akili zako zote na moyo wako wote lazima lifeli.
Na Jambo lolote unalolifanya Kwa mambo hayo matatu lazima lifanikiwe.
Kufanikiwa sio bahati isipokuwa ni Jambo la hakika.
Ukishaanza Kuzuga huwezi kufika popote,
Watu wanaozuga katika maisha huwa na sifa kuu moja, nayo ni VISINGIZIO;
Akiwa shuleni utasikia atakuambia shule haina vitabu, haina waalimu, haina madawati au pengine chakula,
Wote waliozuga shuleni walifeli,
Lakini wasiokuwa na visingizio, huwa na mtazamo kuwa, ILIMRADI SHULE IPO, MIMI LAZIMA NIFAULU.
Na wengi wenye Mitazamo ya hivi walifaulu licha ya uwepo wa changamoto nyingi katika shule hizo.
Watu wanaozuga, wenye visingizio huwa watu wa lawama, na siku zote mtu mwenye kulaumu hana SHUKRANI, na mtu asiye na shukrani lazima maisha yamuumize kivyovyote vile.
Maisha hayahitaji UZUGE na kutoa VISINGIZIO. Maisha yanahitaji kushukuru Yale uliyojaliwa na kuyafanyia kazi ili upate Yale unayoyatamani.
Kujaliwa uzima na Afya, Akili, na kuwa binadamu pekee ni Jambo la kumshukuru MUNGU.
Acha KUZUGA,
Unakuta mtu anafanya biashara Fulani, yaani anafanya Kama kalazimishwa, haipendi kazi yake, Hapendi wateja wake, Hapendi kipato chake ndio maana anakitumia pasipo malengo,
Ukimuuliza atakuambia Mimi nafanya kazi hii basi tuu, ndoto yangu nilitaka kuwa mtu Fulani, huwezi ukafanikiwa Kwa Kuzuga.
Maisha ni vita, sasa Kama wewe upo vitani unazuga subiri misumari ikupige uanze kulia Lia.
Vijana wasomi,
Acheni Kuzuga, FANYENI kazi zozote, msisubiri kwani maisha hayasubiri.
Soma Gap lililopo kwenye jamii yako, kisha ziba Gap Hilo Kwa akili zako zote, moyo wako wote na nguvu zako zote.
Maisha hayaogopi hivyo nawe yakupasa usiwe mwoga, maisha yapo Kwa sababu upo hai, maisha hayapo usipokuwepo, usizuge.
Kufeli hakunaga KISINGIZIO, kufeli ni kufeli, halikadhalika kufaulu hakuna kisingizio.
Ili ufanikiwe lazima uishi, na ili uishi sharti uyafanye maisha yawe wewe, yawe yako, ishi vile unavyotaka uishi, yapeleke maisha unakotaka yaende, na hili ili lifanyike lazima uwe mtu mwenye mipango, jasiri, usiye na woga.
Uwe tayari Kumkabili yeyote Kwa nguvu zote, akili yote na moyo wote, usifanye vitu Nusu nusu, usijaribu Maisha kwani maisha hayajaribiwi isipokuwa Yanafanywa yawe na yanakuwa.
Piga na pigana.
Mkabili yeyote,
Usilaze damu,
Usiwe na visababu na visingizio,
Acha Kuzuga.
Fanya maisha yakulilie, usiyalilie maisha. Fanya maisha yakubembeleze, usiyabembeleze maisha. Fanya maisha yakusubiri, usiyasubiri maisha.
Naomba niishie hapo.
Jumbe hiyo isomwe na wenye akili, wenye maarifa na ufahamu. Hao wapate maana, tena waizalishe maana hiyo iwe machoni mwao na kizazi Chao. Lakini isomwe na wapumbavu kipumbavu, nao wasielewe, wazidi kuchanganyikiwa na kukichanganya kizazi Chao.
Ulikuwa nami;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam.