MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Hakikisha biashara inayokupa kipato inakuwa imara kiasi kwamba ndo inakuwa kama utambulisho wako kwenye jamii kabla ya kufungua nyingine. Kwa mfano kwa sasa likitajwa jina na Bilionea Mulokozi moja kwa moja kinachokujia kichwani ni biashara yake ya pombe za ovyo.
Akitajwa Joseph Kusaga kitakachokujia kichwani ni biashara ya media. Kimsingi hawa watu wawili wana biashara zao zingine ila walihakikisha biashara zao za mwanzo zilizofanya vizuri zimekuwa kubwa na kuimarika. Hata Bill Gates na Microsoft yake amewekeza kwenye kuchimba madini huko Zambia.
Kijana kuwa makini na Motivation Speakers wanaosema usiweke mayai kwenye kikapu kimoja. Unapoanzisha biashara nyingine lazima ikugharimu mtaji na usimamizi. Inawezekana mtaji usiwe shida ila usimamizi ukawa mgumu ukaishia kuathiri hadi biashara ya mwanzo iliyokupa mtaji. Kuliko kukimbilia kufungua biashara mpya bora ufungue tawi la biashara unayofanya kwa sasa kwa sababu usimamizi wake hauwezi kukuzingua.