Acheni kuuza magari kwa kuthaminisha thamani ya gari na NAMBA

Subiri ukutane na namba E kumbe imetoka hapo kisiwa ndui na iliingia Zanzibar 10yrs ago ila nimeivusha bara na kuipa usajiri mpya
Mkuu Nimesema ni njia rahisi sio njia pekee, lazima pia ufuatilie inspection report yake na Grade yake, pia ilisafirishwa lini kutoka Japan. Lakini yote hayo yanaanzia na namba E,

Pia, kuna kampuni/Mashirika Bongo zinanua gari 0 km, wale utakuta registration ni namba C lakini gari ni kinanda na ukiipata kwenye minada ya apa bongo ni sawa na namba F ya used imported, especialy kama hilo shirika linafuta proper maintenance!

Mwisho wa siku tatizo na mafundi Maiko gari ukiitunza haizeekiba Japan Hamna Mamaiko.
 
Uliachoandika ni sahihi kabisa. Kwa mfano ukipata gari zilizotumika ubalozini, mashirika ya kimataifa kama UNDP, UHNCR, UNOPS, WFP, FAO, UNICEF nk, wao huingiza magari yakiwa mapya kabisa na wanafanya service za kueleweka kwa sababu wanatumia mtoa huduma aliye na sifa nzuri kufanya service za magari yao. Ukiyapata hayo minadani hata kama gari lilinunuliwa miaka 7 iliyopita unakuta bado zima sana na huenda hata kilometa 100,000 halijafikisha. Ila tu, mengi ya magari hayo yanakuja bila ushuru (import duty), utalazimika kumalizana na TRA kabla hujalibeba mnadani.
 
sisi wabongo tuna kaushamba fulani kakuzaliwa nako, hatuji kukubali na kubadilika. mtu anachekelea namba mpya ya gari badala ya kuangalia ubora wa gari katika engine, gearbox na body.
 
magari mengine yametumika Zanzibar yameburuzwa ovyo ovyo yakivuka bara yanasajiliwa namba E ya leo, na ushamba wetu wa bara tunazishobokea namba ndo gari mpya.
 
Subiri ukutane na namba E kumbe imetoka hapo kisiwa ndui na iliingia Zanzibar 10yrs ago ila nimeivusha bara na kuipa usajiri mpya
Canter town ace na mende nyingi zinatoka zenji zimepiga kazi huko zaidi ya miaka 20 zinaletwa na usajili wa E bara tunaziita mpya
 
siku yako ikifika utajua haujui
 
Gari imekaa zanzibar miaka 20 ikija bara mnaita mpya kwa namba E zanzibar nayo ni bongo imejaa gari mbovu na chakavu
 
Gari imekaa zanzibar miaka 20 ikija bara mnaita mpya kwa namba E zanzibar nayo ni bongo imejaa gari mbovu na chakavu
Lakini kwenye karatasi si unaona kabisa huu mzigo umetokea zanzibari hapo kwa hamii halunde.. 😂
 
Kuna mzee ana IST yake ya namba D huwa anipaki ndani tu mara nyingi anatumia VX lake kwenye mishe zake. Alikuwa anaitumia IST kipindi cha Corona na ni mara chache sana jioni.

Nadhani alipitia msuko suko wa uchumi kipindi kile ila sasa amekaa sawa amerudia uchumi wake wa zamani.

Zile gari zinapaki kwenye shade ukipita muda wote ile IST unaikuta imepaki na nikinanda balaa ukipishana nayo unajua hii gari ipo kwenye hali nzuri kuanzia engine hadi body vimekaza balaa.

Sasa mzee kama huyu akisema anakuuzia hii gari ukiangalia namba utakuwa ni mjinga sababu ubora wa hii gari ni wa kiwango cha juu sana.
 
kununua gari..unahitaji kuunganisha facts ndogo ndogo nyingi, ili upate kitu kimoja.. Number ikiwa mojawapo... Barabara za bongo, zinafahamika , hata ungekuwa mtunzaji kiasi, utaliwa na kutu ya barabara mbovu zenye mashimo na kujaa mabwaa ya maji....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…