Hilo halikubaliki kabisa kabisa ,kwani sio ustaarabu wa kufanya siasa naona waliofanya hivyo watakuwa wamejidharau wenyewe na wamekosa uvumilivu wa kisiasa au wameshindwa na akili zao zinaonyesha wazi wazi ni finyu ,mimi wakati wa kampeni huwa nauona kama wakati wa mavuno kuna watu wanajenga ,kuna watu wanatajirika wakati huu na kuna watu wanapata hela wakati huu na wengi wa hao hawajali wanapokea hela au kitu,au tuseme zawadi kutoka chama gani, jamani siri ya mpiga kura anaijua mtu mwenyewe ,wakati wa kampeni huwa tunasema ukipewa hela pokea na kula,ukipewa ngua chukua na ivae ,hivi jamani hapa JF zitembezwe milioni mojamoja kwa cheque ,iwe inatoka CCM ,au Chadema au CUF au kwengine kokote kule mtazikataa ,mimi nitachukua na kura yangu nitaipeleka ninapoitaka na kama kofia na fulana nitazivaa vile vile ,muhimu msimamo wangu haubadiliki, Sasa tuchukue picha ya mgombea wako amevalishwa huyo jibwa ,wewe utahisi vipi ? Hilo kwa kweli halikubali na kamuulize huyo kiongozi wako uone jibu atakalo kupa na akikwambia inafaa basi hafai kuwa kiongozi hata wa timu ya gololi.