Achoma gari makusudi baada ya kushindwa kulipa deni la gari hilo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
POLISI mkoani Morogoro inawashikilia watu watatu akiwemo mmiliki wa basi la kampuni ya HBD lenye namba za usajili T 321 DKW, Ahmedi Hemed (25), kwa tuhuma za kuchoma moto basi hilo na kusingizia kuwa moto huo ulitokana na matatizo ya mfumo wa breki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amesema kuwa watuhumiwa hao walikula njama ya kufanya tukio hilo baada ya mmiliki kushindwa kulipa deni la basi hilo kwa moja ya taasisi za fedha nchini linalodaiwa kufikia zaidi ya sh. milioni 200.

 
Duuuuuuu....kuna mwengine uku kwetu nae kachoma nyumba yake kukwepa deni la bank.
🀣 🀣 🀣 sasa anaikomoa bank ama anajikomoa mwenyewe?
 
Hio imekula kwake mazima,basi umechoma na bado deni limesimama
 
[emoji1787][emoji1787]
 
Hapo bima wamewahi polisi na kuwapoza..
 
Hilo basi lililounguzwa, lilikuwa na mfumo gani wa matairi, triplet kama semi trailer?

Basi gani la hivyo, au ili mradi wameweka tu picha ya gari lililoungua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hadi huruma. Inaonekana hakuwa mzoefu kwenye haya mambo.

Angekula na:
Polisi
Fire
Bima
Kisha na hao wanaomdai.

Hapo issue ingeisha juu kwa juu.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
sasa hapo kwenye picha mbona linaonekana hakuna diff wala fron axle pia hata viti hakuna


unadhani itakuwa ni rahisi kucheza dili kihivyo?
 
Utajiri huu....!!![emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Hii si ilikuwa ally star ndo iliungua majuzi tu watu wakatoa mizigo yote.

Kacheza betting ila kaliwa yeye dah, maana angeletewa mchuma mpyaa na Bima ila ndo kasha kula kekundu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…