Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Amani
Na Mwandishi Wetu
Mkazi mmoja wa Manzese Argetina, jijini Dar es Salaam, aliyetambuliwa kwa jina la Richard Epro (28), amechomwa kisu mbavuni na kijana mwenzake aliyejulikana kwa jina la Calvin Henry baada ya kukataa kumuuzia kipisi cha bangi... Akiongea na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita, shuhuda mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kwamba, Richard ambaye ni muosha magari katika Kituo cha Mabibo Mwisho, anadaiwa kuwa anafanya biashara ya bangi akishirikiana na wenzake.
Calvin alifika hapa Mabibo majira ya mchana na kumkuta Richard akiwa bize na kazi yake ya kuosha gari, akamtaka amuuzie bangi, lakini kijana huyo alimkatalia akidai kuwa anayefanya biashara hiyo hakuwepo na kwamba yeye si muhusika. Jamaa alipoambiwa hivyo akasema hataki kusikia maneno hayo hivyo kumlazimisha amuuziwe, alisema shuhuda wetu.
Aliongeza kuwa, Richard alipoona anazidi kusumbuliwa huku akiwa kazini, aliamua kumsukuma akijua labda litakuwa ndiyo suluhisho la Calvin kuondoka lakini badala yake, aliangukia kwenye mtaro wa maji machafu na ndipo balaa lilipoanza.
Baada ya kuona kasukumwa na kuangukia kwenye mtaro wa maji machafu, Calvin alinyanyuka na kutoa kisu kisha kumchoma nacho Richard mbavuni na kumsababishia kutokwa na damu nyingi na alipoona hali hiyo alianza kutimua mbio lakini majeruhi alijitahidi kupiga yowe za mwizi, ndipo watu wakajitokeza na kumsaidia kumkamata mtuhumiwa, alisema shuhuda huyo.
Alisema mtuhumiwa aliponyoka na akakimbilia katika ghorofa B la Urafiki ambapo alipanda juu lakini wananchi walimfuata huko na kufanikiwa kumkamata na kumteremsha chini kisha wakamfikisha Kituo cha Polisi Urafiki na kuwekwa rumande.
Habari zinasema, baadaye polisi walifika eneo la tukio wakamchukua majeruhi wakampeleka kutibiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Mganga mkuu wa hospitali hiyo alishauri apelekwe Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na jeraha lake alilolipata kuwa kubwa, alisema mtoa habari huyo.
Hadi tunakwenda mtamboni, polisi walithibitisha kuwa mtuhumiwa alikuwa bado anashikiliwa katika Kituo Cha Polisi Urafiki akisubiri kufikishwa mahakamani.